Mamlaka ya usimamizi wa bandari nchini imekusudia kurasimisha bandari bubu zaidi ya 250 zilizopo hapa nchini ili kuongeza wigo wa mapato yatokanayo na bandari.

Mamlaka ya usimamizi wa bandari nchini imekusudia kurasimisha bandari bubu zaidi ya 250 zilizopo hapa nchini ili kuongeza wigo wa mapato yatokanayo na bandari ambapo bandari hizo zinaweza kuchangia karibia nusu ya mapato yote yatokanayo na bandari ya Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari ofsini kwake mkurugenzi wa mamlaka ya usimamizi wa bandari nchini TPA mhandisi Deusdediti Kakoko amesema kuwa Tanzania ina bandari bubu takribani mia tatu ambazo zote zikitambuliwa na kurasimishwa rasmi zinaweza kuongezea mapato serikali na kwamba mapato yatokanayo na bandari hizo yanaweza kufikia nusu ya mapato yote ya bandari ya Dar es Salaam

Aidha Mhandisi Kakoko anasema kuwa uamzi wa kuzirasimisha bandari hizo ni kutokana na sababu za kiuslama kwa kuwa bandari nyingi zipo mpakani mwa nchi.

Comments

comments