Bei zao la Kakao katika Wilaya ya Kyela Mkoani Mbeya imeendelea kuongezeka kutoka shilingi 3,700 katika gulio la kwanza hadi kufikia shilingi 4,675 kwa kilo moja

Bei zao la Kakao katika Wilaya ya Kyela Mkoani Mbeya imeendelea kuongezeka kwenye minada inayoendelea kufanyika , kutoka shilingi 3,700 katika gulio la kwanza hadi kufikia shilingi 4,675 kwa kilo moja na hivyo kuleta tija kwa wakulima wa zao hilo.

Channel ten imefika kwenye mnada wa Kakao ambao umeendeshwa katika Wilaya ya Kyela na kushindanisha makampuni mbalimbali, huu ukiwa ni mnada wa tano tangu kuanza kwa msimu wa uuzaji wa Kakao, ambapo awali mnada wa kwanza kakao imeuzwa kwa shilingi 3700, Mrajisi Msaidizi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Mbeya Angela Maganga anawataka wakulima kuwa na kokoa bora.

Baadhi ya makampuni ambayo yameshindanishwa na kushindwa kwenye mnada huu wamepongeza uendeshwaji wake kuwa ni huru na haki.Kampuni ya Mohamed Interprise imeshinda mnada huu kwa kununua tani laki 219,175 za kakao kwa shilingi 4,675 kwa kilo, huku bei elekezi ikiwa ni shilingi 3200.

Comments

comments