Benki Kuu ya Tanzania BOT imezitaka taasisi za fedha nchini yakiwemo mabenki kuongeza ubunifu kwenye matumizi ya teknolojia za kigitali ili kurahisishi huduma kwa wateja.

Benki Kuu ya Tanzania BOT imezitaka taasisi za fedha nchini yakiwemo mabenki kuongeza ubunifu kwenye matumizi ya teknolojia za kigitali ili kurahisishi huduma kwa wateja, hatua itakayookoa muda mwingi wa kufuatilia huduma hizo kutoka sehemu moja kwenda nyingine.

Naibu Gavana wa BOT Dkt. Bernard Kibesse ametoa wito huo wakati akizungumza kwenye uzinduzi wa mfumo mpya wa matumizi ya Teknolojia ya kidigitali uliobuniwa na Benki ya Standard Chatered Tanzania, mfumo ambao utawawezesha wateja kupata huduma zaidi ya 70 kwa kujihudumia wenyewe popote walipo.

Awali Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Sanjay Rughani alisema mfumo huo ni mwendelezo wa kurahisisha upatikanaji wa huduma kupitia matumizi ya teknolojia za kidigitali kulingana na mapinduzi ya mifumo ya kimataifa ya utoaji wa huduma za kibenki katika kukidhi matakwa ya wateja.

Mfumo uliozinduliwa unayo programu inayoweza kupakuliwa ama kuboreshwa kupitia simu za kisasa za google play store ama apple store ambapo pamoja na mambo mengine, mtumiaji anaweza kufungua akaunti kwa njia ya mtandao ndani ya muda usiozidi dakika kumi na tano.


Comments

comments