Bonanza la watoto Lindi, Afya na Ukakamavu vyawa kichocheo

eee

Mkuu wa wilaya ya Lindi, Shaibu Ndemanga amemuagiza mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya pamoja manispaa ya mji wa Lindi kurejesha viwanja vyote vilivyotengwa kwa ajili ya michezo mashuleni ili watoto wapate fursa ya kuonyesha vipaji vyao ikiwemo michezo ya sanaa.

Akihutubia wazazi na wanafunzi wa shule za msingi zilizo katika manispaa ya lindi leo,mara baada ya kufunga mashindano ya michezo kwa shule 10 za msingi kwa ajili ya uhamasishaji wazazi kuhakikisha wanachangia watoto kupata huduma bora za afya kupitia mpango wa TOTO AFYA KADI unaosimamiwa na Mfuko wa NHIF

Pamoja na kushuhudia mchezo wa fainali uliomalizika kwa shule ya msingi mpilipili kutwaa ubingwa huo baada ya kuichapa shule ya msingi mitwero kwa mabao 2 kwa Moja,Ndemanga alitumia fursa kuwaasa wazazi kutoa mwanya kwa watoto kucheza huku akieleza mpango wa serikali kuboresha viwanja vya michezo kwa kuzitaka taasisi mbalimbali kuunga mkono jitihada hizo ikiwemo michezo ya bonanza

Pamoja na zawadi na msaada huo wa matibabu baadhi ya wanafunzi walitumia fursa ya uwepo wa channel ten kushukuru mpango huo wa kuhamasisha wazazi afya kwa watoto huku wakiomba kuanzishwa kwa Academy za michezo katika mkoa wa lindi

Comments

comments