Benki Kuu ya Tanzania BOT imeyaambia mabenki nchini kuwa ubunifu katika kutoa huduma uhakikishe huduma hizo zinawafikia wananchi wa vijijini, badala ya kuwanufaisha wakazi wa mijini pekee.

Rai hiyo imetolewa na Meneja wa Mifumo ya Benki Kuu Bw. Thomas Mongela, wakati wa uzinduzi wa huduma inayoitwa Magic Banking, iliyobuniwa na Benki ya Uba jijini Dar es Salaam.

Bw. Mongela amesema licha ya ushindani uliopo kwenye sekta ya benki nchini, huduma za kibenki hazijawafikia wananchi wa vijijini kwa kiwango cha kutatua changamoto zilizopo, hivyo ubunifu wa kurahisisha huduma ni muhimu zikawagusa pia wananchi wa vijijini.

Awali Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi na Huduma za Kimtandao Bw. Asupya Nalingigwa alisema huduma iliyozinduliwa itatumia mitandao ya simu kwa wateja kufanya shughuli zote za kibenki kwenye simu za aina yoyote.

Comments

comments