Wakaazi wa Beni, Butembo na Yumbi wanaendelea kusubiri matokeo ya uchaguzi wa wabunge DRC.

Wakaazi wa Beni, Butembo na Yumbi wanaendelea kusubiri matokeo ya uchaguzi wa wabunge uliyofanyika jana¬† Machi 31 baada ya kuahirishwa miezi mitatu iliyopita. Uchaguzi huo umefanyika katika maeneo hayo matatu, baada ya Tume ya Uchaguzi (CENI) kuchukuwa hatua ya kusogeza mbele uchaguzi katika maeneo hayo kutokana na sababu za kiusalama na afya. Wapiga kura katika[…]

Rais wa Comoro aliyepo madarakani Azali Assoumani anayetetea kiti hicho anatarajiwa kuchaguliwa tena kufuatia uchaguzi uliofanyika jana visiwani humo.

Hata hivyo wapinzani wamelalamikia uchaguzi huo kwa madai kuwa kumekuwa na dosari nyingi kwenye vituo kadhaa vya kupigia kura ambazo wamezilalamikia kwa tume ya uchaguzi . Kiongozi wa kampeni za Rais Azali amesema wapinzani wamesababisha hali ya taharuki kwa lengo la kuvuruga mchakato wa uchaguzi licha ya kwamba uchaguzi huo umefanyika katika hali ya kawaida.[…]

Maelfu ya watu wamekusanyika kote nchini New Zealand kufanya ibada maalumu ya kuwoambea wale wote walipoteza maisha katika shambulizi la kigaidi lililoua watu 50 na wengine kadhaa kujeruhiwa ambalo lilitokea kwenye misikiti miwili katika mji wa Christchurch.

Waombolezaji, wengi wao wakiwa wamefunika vitambaa kichwani, walikusanyika katika uwanja wa Hagley Park, mkabala na msikiti wa al-Noor ambako watu 42 waliuawa ambapo baada ya sala, kukawa na kimya cha dakika mbili. Kote nchini humo, maelfu ya watu walishiriki sala hiyo, ambayo ilirushwa moja kwa moja kwenye vituo vya redio na televisheni. Ijumaa iliyopita, mtu[…]

Ripoti mpya kutoka Umoja wa Mataifa na serikali za nchi tatu za kusini mwa Afrika zilizoathirika na Kimbunga Idai zinasema bado watu wengi wako katika uhitajiwa wa chakula na malazi huku idadi ya vifo ikiripotiwa kupanda.

Afisa wa Umoja wa Mataifa anasema Kimbunga Idai kimeuwa mamia kwa maelfy ya watu katika chi ya Msumbiji, Malawi, na Zimbabwe na pia kimeharibu miundombinu ya barabara na umeme katika nchi hizo. Maafisa nchini Msumbiji wanasema watu zaidi ya 15,000 wanahitaji kuokelewa haraka na kupewa hifadhi kutokana na kimbuga hicho kilichopewa jina la Idai, kilichosababisha[…]

Baadhi ya raia wa Msumbiji wanakabiliwa na ukosefu wa umeme na maji siku chache baada ya kimbunga Idai kupiga baadhi ya maeneo ya nchi hiyo na kuharibu kabisa miundombinu ya huduma hizo.

Habari zinasema idadi ya waliopoteza maisha kutokana na maafa hayo huenda ikafika watu 1,000. Kimbunga Idai kiliuathiri zaidi mji wa Beira ambapo Shirika la Msalaba Mwekundu na shirika Hilal Nyekundu yameripoti kwamba asilimia 90 ya majengo yameharibiwa vibaya na kupoteza kabisa taswira ya mji huo wa Beira huku miili mingine ya watu ikiendelea kupatikana katika[…]

Hali ya tahadhari imetangazwa nchini Zimbabwe katika maeneo yaliyoathiriwa na kimbunga Idai kilichokumba maeneo mbalimbali nchini humo kikiwa na mwendo kasi wa kilomita 177 kwa saa.

Mpaka kufikia leo imeripotiwa kwamba watu 65 ndio walipoteza maisha Mashariki mwa Zimbabwe kutokana na eneo hilo kukumbwa na kimbunga hicho. Rais Emmerson Mnangagwa amelazimika kusitisha ziara yake mashariki ya kati ili kurejea nchini mwake kutokana na janga hili. Jitihada za uokoaji zinaendelea huku mamia ya watu wakiwa hawajulikani walioko,hali inahofiwa kwamba huenda inaweza ongeza[…]

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, Felix Tshisekedi amewasamehe takriban wafungwa 700 wa kisiasa waliofungwa jela na utawala wa mtangulizi wake, Joseph Kabila.

Tshisekedi alisaini amri ya rais ya kuwasamehe wafungwa hao jana na kutimiza ahadi aliyoitoa mwanzoni mwa mwezi huu, kwamba hilo ni moja kati ya mambo atakayoyafanya katika siku zake 100 za kwanza madarakani. Miongoni mwa walioachiwa huru ni Firmin Yangambi, aliyehukumiwa mwaka 2009 kifungo cha miaka 20 gerezani kwa makosa ya kutishia usalama wa taifa.[…]

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema ili kuibadili Afrika Viongozi wake lazima wawekeze kwa Vijana na Watoto.

Makamu wa Rais ameyasema hayo wakati akihutubia kwenye mkutano wa Africa Now Summit 2019 jijini Kampala nchini Uganda. Amesisitiza kwamba viongozi lazima wawekeze kwenye Lishe bora ya watoto wanaozaliwa na kuhakikisha mifumo ya elimu inalenga kutoa elimu bora na zenye kukuza vipaji ili kwenda sambamba na ulimwengu wa teknolojia. Aidha Makamu wa Rais amesisitiza Afrika[…]