ecff50a140ea64e9ba24d0ca5a185df5

Mgogoro wa Kisiasa DRC Congo, Viongozi wa kanisa katoliki nchini humo wawtaka wananchi kuendelea kudai haki

Kanisa Katoliki nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, limewataka raia wa nchi hiyo kutokata tamaa katika harakati za kutafuta haki ya kisiasa nchini humo, pamoja na kupigania haki zao. Kauli hii imetolewa na Baraza la Maaskofu wa Kanisa hilo CENCO, ambao wana unashawishi mkubwa wa kisiasa nchini humo. Msemaji wa CENCO Padri Donatien Nshole, amesema[…]

DTQeWSRW0AA-PRl

Baada ya Vurugu na maandamano nchini Tunisia, Serikali yatangaza azma ya kuzidisha misaada kwa jamii masikini

Serikali ya Tunisia imetangaza azma ya kuzidisha misaada kwa jamii ya watu wasiokuwa na uwezo. Uamuzi huo umepitishwa kufuatia wimbi la maandamano na machafuko dhidi ya hatua za kuzidisha bei za vitu na kodi za mapato. Waziri wa masuala ya jamii Mohammed Trabelsi amesema misaada ya jamii itaongezeka na kufikia Euro milioni 60 ambapo familia[…]

US-POLITICS-TRUMP

Umoja wa Afrika,Wamtaka rais Trump kuomba radhi kwa kutoa matamshi ya kibaguzi dhidi ya mataifa ya Afrika

Uongozi wa Umoja wa Afrika unaowakilisha nchi 54 za Afrika umemtaka Rais wa Marekani Donald Trump kuziomba radhi baada ya kuripotiwa kutumia maneno machafu alipokuwa akizungumzia kuhusu wahamiaji kutoka mataifa ya Afrika, Haiti na El Salvador wakati alipokutana na wabunge Ikulu. Baada ya kikao cha dharura cha mabalozi wa nchi za Afrika katika Umoja wa[…]

Hatua ya kubakia madarakani kwa rais Gabon, Hatimaye wabunge nchini humo wabadilisha katiba ya nchi hiyo

Wabunge nchini Gabon wamebadilisha Katiba ya nchi hiyo, na kuondoa ukomo wa mihula kwa rais, kinyume na ilivyokuwa awali ambapo alihudumu kwa mihula miwili, kila muhula miaka saba. Hii inamaanisha kuwa rais wa sasa Ali Bongo anaweza kusalia madarakani kwa muda mrefu iwapo atachaguliwa tena na raia wa nchi hiyo utakapofanyika tena uchaguzi mkuu. Mabadiliko[…]

2018-01-09t144221z_220142249_rc172d21cb40_rtrmadp_3_tunisia-protests_0

Vurugu Nchini Tunisia, Wizara ya mambo ya ndani yasema takriban maofisa polisi 50 wamejeruhiwa

Wizara ya mambo ya ndani ya Tunisia imesema kwamba takriban maafisa wa polisi 50 walijeruhiwa katika machafuko yanayoendelea nchini humo huku ikiripotiwa kwamba watu 300 wamekamatwa kufuatia vurugu hizo. Machafuko hayo yametokanana na watu wanaoandamana kupinga ongezeko la bei na hatua za kubana matumizi. Katika mji wa Thala, ulio karibu na mpaka na Algeria, waandamanaji[…]

39971287_303

Ripoti ya EU kuhusu Uchaguzi wa Kenya, Waangalizi wasema uchaguzi ulikumbwa na karoso

Waangalizi wa uchaguzi wa Umoja wa Ulaya wamesema kuwa uchaguzi wa urais nchini Kenya uliokumbwa na kasoro, umeidhoofisha demokrasia ya nchi hiyo. Wamesema hayo katika ripoti ambayo hata hivyo imekosolewa vikali na serikali ya Kenya. Rais Uhuru Kenyatta alishinda uchaguzi wa marudio mwezi Oktoba baada ya ushindi wake wa awali kaitika uchaguzi wa Agosti kubatilishwa[…]

120189133049275241480

Hali ya Machafuko nchini Tunisia, Zaidi ya watu mia mbili wamekamatwa kufuatia fujo zilizoibuka baada ya maandamano

Kumekuwa na muendelezo wa siku tatu za ghasia za maandamano nchini Tunisia katika mji mkuu wa Tunis na miji mingine ya nchi hiyo. Polisi wamekuwa wakuirusha mabomu ya machozi kwa kundi kubwa la watu ambao wamekuwa wakilalaika juu ya mfumko wa bei ambao unaathiri upatikanaji wa mahitaji muhimu. Hata hivyo Waziri mkuu Yousef Chahed amelaani[…]

13-1

Mgogoro wa DRC CONGO,Baraza la usalama la umoja wa Mataifa lakutana tena

Baraza la Usalama la Umoja wa Matifa linakutana leo kujadili hali tete inayojiri katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambako uchaguzi mkuu unatarajiwa kuandaliwa mwishoni mwa mwaka huu. Wiki iliyopita, Umoja wa Mataifa ulisema unatiwa wasiwasi mkubwa na vitendo vya vikosi vya usalama nchini humo vinavyofanywa dhidi ya waandamanaji wanaomtaka Rais Joseph Kabila kuachie madaraka.[…]

16018716_303

Maandano kupinga mfumko wa bei Tunisia,Mtu mmoja auawa na wengine watano kujeruhiwa

Kumekua na maandamano katika mji mkuu wa Tunisia, Tunis, kufuatia mfumko wa bei, maandamano ambayo yamesababisha kifo cha mtu mmoja na wengine watano wamejeruhiwa. Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini Tunisia, maandamano hayo sasa yameenea katika maeneo mengine nchini humo ambapo inaelezwa kuwa sababu ya maandamano hayo ni mfumko wa bei ambao umesababisha kuongezeka[…]