Mchumi na mhadhiri kutoka Chuo Kikuu Mzumbe Profesa Honest Prosper Ngowi amepongeza makadirio ya Bajeti kwa mwaka 2019/20 pamoja na vipaumbele vyake pamoja na kusisitiza umuhimu wa kuendelea kukuza mapato ya ndani.

Mchumi na mhadhiri kutoka Chuo Kikuu Mzumbe Profesa Honest Prosper Ngowi amepongeza makadirio ya Bajeti kwa mwaka 2019/20 pamoja na vipaumbele vyake pamoja na kusisitiza umuhimu wa kuendelea kukuza mapato ya ndani ili nchi iweze kujitegemea na kupunguza au kuachana kabisa na fedha za wahisani. Akitoa uchambuzi wa makadirio ya bajeti hiyo Profesa Honest Prosper[…]

Kampuni ya Africa Media Group wamiliki wa Kituo cha Television cha Channel Ten na Radio Magic Fm imezindua nembo ya maonesho ya Taasisi za kifedha na Bima (Banking Finance and Insurance Expo 2019).

Kampuni ya Africa Media Group wamiliki wa Kituo cha Television cha Channel Ten na Radio Magic Fm imezindua nembo ya maonesho ya Taasisi za kifedha na Bima (Banking Finance and Insurance Expo 2019) yenye lengo la kutaka kufahamisha wananchi hasa wa Dodoma nini taasisi hizo zinafanya sambamba na kujua fursa zilizopo katika Taasisi hizo na[…]

Benki Kuu ya Tanzania BOT imezitaka taasisi za fedha nchini yakiwemo mabenki kuongeza ubunifu kwenye matumizi ya teknolojia za kigitali ili kurahisishi huduma kwa wateja.

Benki Kuu ya Tanzania BOT imezitaka taasisi za fedha nchini yakiwemo mabenki kuongeza ubunifu kwenye matumizi ya teknolojia za kigitali ili kurahisishi huduma kwa wateja, hatua itakayookoa muda mwingi wa kufuatilia huduma hizo kutoka sehemu moja kwenda nyingine. Naibu Gavana wa BOT Dkt. Bernard Kibesse ametoa wito huo wakati akizungumza kwenye uzinduzi wa mfumo mpya[…]

Serikali imeruhusu wafanyabiashara wenye vibali vya kuagiza sukari kutoka nje ya nchi kuendelea kufanya hivyo siku chache tangu wizara ya kilimo kueleza nia yake ya kusitisha uagizaji wa sukari kutoka nje kwa wazalishaji wa ndani.

Serikali imeruhusu wafanyabiashara wenye vibali vya kuagiza sukari kutoka nje ya nchi kuendelea kufanya hivyo siku chache tangu wizara ya kilimo kueleza nia yake ya kusitisha uagizaji wa sukari kutoka nje kwa wazalishaji wa ndani, baada ya majadiliano kati ya wazalishaji hao na wizara ya kilimo. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam[…]

Waziri Kakunda, amewahimiza Watanzania kupanda mazao yanayoondoa umasikini ikiwemo Miparachichi, kwani ukiweza kulima zao hilo unaweza kuvuna katika maisha yako yote.

Waziri wa Viwanda na Biashara Joseph Kakunda, amewahimiza Watanzania kupanda mazao yanayoondoa umasikini ikiwemo Miparachichi, kwani ukiweza kulima zao hilo unaweza kuvuna katika maisha yako yote. Waziri Kakunda akiendelea na ziara yake Wilayani Siha Mkoani Kilimanjaro, alipata fursa ya kutembelea Kiwanda cha Africado, kinachozalisha miparachichi , ambapo amewahamasisha watanzania kujijengea utaratibu wa uthubutu kwa kununua[…]

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa wakulima wa alizeti mkoani Singida kutumia mkopo walioupata kutoka Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB).

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa wakulima wa alizeti mkoani Singida kutumia mkopo walioupata kutoka Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) ili kuendeleza uzalishaji wa mazao ya kimkakati mkoani humo. Makamu wa Rais ametoa wito huo wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara wa kukabidhi hundi ya mfano yenye thamani[…]

Shirika la viwango Tanzania TBS limeteketeza tani 4.5 za bidhaa mbalimbali zenye thamani ya Shilingi Milioni 67, baada ya kubainika kuwa na viwango hafifu vya ubora.

Bidhaa zilizotekezwa ni pamoja vifaa vya kuzuia majanga ya hitilafu za umeme na radi majumbani (earth copper), vijiko vinavyotumika kwa matumizi ya nyumbani kama vile kulia chakula, pamoja na makufuli ambavyo vilikamatwa February 2 mwaka huu katika bandari ya Dar es salaa vikiingizwa nchini kutokea China. Afisa Ubora wa Viwango wa TBS Grangay Masala aliyesimamia[…]

Shirika la Mawasiliano Tanzania TTCL limepewa siku 30 kuhakikisha maeneo yote ambayo hayana kadi za simu na vocha za simu za mtandao huo zinawafikia.

Akizungumza alipotembelea makao makuu ya shirika hilo jijini Dar es Salaam, Naibu Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi Mhandisi Atashasta Nditiye amesema haifai kuona maeneo ya vijijini bado hayapati huduma za mawasiliano kwa ufanisi. Naibu Waziri Nditiye ametoa mwezi moja kwa shirika hilo kutatua changamoto ya upatikanaji wa kadi za simu pamoja na vocha za simu[…]

Waziri Angela Kairuki amesema serikali inaendelea kuboresha mazingira ya Uwekezaji kwa Wawekezaji na Wafanyabishara wa ndani na nje ya nchi.

Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji Angela Kairuki amesema serikali inaendelea kuboresha mazingira ya Uwekezaji kwa Wawekezaji na Wafanyabishara wa ndani na nje ya nchi pamoja na kuhakikisha vikwazo vilivyokuwa vinawakabili ikiwemo urasimu katika utoaji vibali na upatikanaji wa ardhi vinatokomezwa. Waziri Kariuki pia ametoa rai kwa Watanzania wenye maeneo makubwa ya ardhi[…]