Wizara ya Madini kwa kushirikiana na Taasisi ya uongozi nchini, imewakutanisha wadau wa sekta ya madini kujadili kanuni za Sheria ya madini ya mwaka 2017, ili rasilimali hiyo iweze kuwanufaisha Watanzania.

Katika kikao hicho kinachoketi Jijini Mwanza, shabaha kubwa inalenga kuimarisha soko la Madini, ili rasilimali hiyo iweze kuchangia kikamilifu katika pato la Taifa, baada ya kubainika kuwa bado kuna wimbi kubwa la utoroshaji wa madini hapa nchini. Kutokana na mjadala huo inategemewa kuwa, hii itakuwa ni neema kwa wachimbaji wadogo pia kupata soko la uhakika,[…]

Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) imewatoa hofu wakulima juu ya soko la mazao ya nafaka, na kuwasisitiza wahakikishe ubora wa mazao yao, kwa kuwa soko la uhakika lipo.

Uhakika huo umetolewa jijini Dodoma na Kaimu Mtendaji Mkuu wa (NFRA) BIBI VUMILIA ZIKANKUBA, wakati taasisi hiyo ikiendesha operesheni ya uuzaji wa tani 36,000 za mahindi na mtama, kwa Mpango wa Chakula Duniani (WFP). Naye, Mkuu wa Kitengo cha Usafirishaji (WFP) BW. MAHAMUD MABUYU, akachukua wasaa kufafanua ni maeneo gani yenye uhaba wa chakula, ambapo[…]

TRA mkoani Njombe imeyakamata malori sita yaliyokuwa yakisafirisha bidhaa za mbao na mkaa kwa tuhuma za kutokuwa na risiti za EFD.

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) mkoani Njombe imeyakamata malori sita yaliyokuwa yakisafirisha bidhaa za mbao na mkaa kwa tuhuma za kutokuwa na risiti za EFD kitendo ambacho kinadaiwa kuwa na lengo la kukwepa kulipa kodi. Meneja wa Mamlaka ya Mapato (TRA) mkoa wa Njombe, Musibu Shabani akizungumza katika eneo la tukio la ukaguzi wa magari[…]

Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imetangaza kuhamisha mali na madeni ya Benki M kwenda Azania Bank Limited.

Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imetangaza kuhamisha mali na madeni ya Benki M kwenda Azania Bank Limited na kwamba kwa sasa Benki Kuu, Benki ya Azania pamoja na wadau wengine wanaendelea kuandaa taratibu za kisheria kukamilisha mchakato wa uhamishaji wa mali na madeni hayo. Akitangaza hatua hiyo kwa waandishi wa habari kwa niaba ya gavana[…]

Benki Kuu ya Tanzania BoT imewashauri viongozi wa taasisi za fedha kuhakikisha wafanyakazi wao wanashiriki mafunzo maalum yaliyoandaliwa kwa njia ya mtandao na Taasisi ya mabenki Tanzania – TIOB .

Benki Kuu ya Tanzania BoT imewashauri viongozi wa taasisi za fedha kuhakikisha wafanyakazi wao wanashiriki mafunzo maalum yaliyoandaliwa kwa njia ya mtandao na Taasisi ya mabenki Tanzania – TIOB kwa kushirikiana na Kampuni ya Kentara Analytics ya Marekani lengo likiwa kuwajengea uwezo wafanyakazi wa benki kukabiliana na mikopo chechefu. Mwakilishi kutoka Benki Kuu ya Tanzania[…]

Rais wa shirikisho la Vyama vya Uchimbaji wa Madini Tanzania John Wambura Bina amewataka wadau wa sekta hiyo kuunga mkono jitihada za Rais John Pombe Magufuli za kulinda rasilimali za taifa yakiwemo madini.

Rais wa shirikisho la Vyama vya Uchimbaji wa Madini Tanzania John Wambura Bina amewataka wadau wa sekta hiyo kuunga mkono jitihada za Rais John Pombe Magufuli za kulinda rasilimali za taifa yakiwemo madini ili kuifanya sekta hiyo kuwa mkombozi wa uchumi kwa wachimbaji na taifa kwa ujumla. Bw. Bina ametoa rai hiyo wakati wa ziara[…]

Katika kipindi cha miezi sita ya mwaka wa fedha 2018/19 ikiwa ni kuanzia mwezi Julai hadi Desemba 2018, TRA imefanikiwa kukusanya jumla ya shilingi trilioni 7.99.

Taarifa hiyo imetolewa na mkurugenzi wa huduma na elimu kwa mlipa kodi TRA Richard Kayombo, ambapo amesema kiasi hicho ni sawa na ukuaji wa makusanyo wa asilimia 2.01 ikilinganishwa na shilingi trilioni 7.83 ambazo zilikusanywa kipindi kama hicho katika mwaka wa fedha wa 2017/18. Amesema makusanyo hayo ya mwezi Desemba yamevunja rekodi kwa kuzidi makusanyo[…]

Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni jijini Dsm imekamilisha zoezi la Kugawa vitambulisho vya wafanyabiashara wadogo maarufu machinga.

Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni jijini Dsm imekamilisha zoezi la Kugawa vitambulisho vya wafanyabiashara wadogo maarufu machinga wenye mitaji isiyozidi shilingi Millioni 4 vilivyotolewa na Rais Dk.John Magufuri siku za hivi karibu ikiwa ni mpango wa kuwatambua wafanyabiashara hao. Mkuu wa wilaya ya Kigamboni Sarah Msafiri akizungumza na waandishi wa habari amesema zoezi hilo la[…]

Serikali imesema imeamua kuondoa baadhi ya tozo mbalimbali zilizokuwa zinakwaza wafanyabiashara baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa baraza la wafanyabiashara ili kutengeneza mazingira wezeshi kwa wawekezaji.

Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu sera, bunge, kazi, vijana, ajira na wenye ulemavu Jenista Mhagama amesema hayo jijini dsm alipotembelea wakala wa usalama na afya mahala pa kazi OSHA na kusema zipo baadhi ya tozo ambazo zilionekana kukwaza shughuli za uwekezaji ambazo zimeondolewa ikiwemo tozo ya usajili iliyokuwa inagharimu kuanzia sh.elf 60 hadi[…]

Mkuu wa wilaya ya Temeke Felix Lyaniva leo amezindua zoezi la Ugawaji vitambulisho kwa ajili ya wafanyabiashara wadodo wadogo maarufu machinga,Mama lishe pamoja na wajasiriamali

Mkuu wa wilaya ya Temeke Felix Lyaniva leo amezindua zoezi la Ugawaji vitambulisho kwa ajili ya wafanyabiashara wadodo wadogo maarufu machinga,Mama lishe pamoja na wajasiriamali huku akiwaasa wafanyabiashara hao kutotumika vibaya na wafanyabiashara wakubwa kwa nia ya kukwepa kodi ya serikali. Akizungumza wakati wa zoezi hilo ambalo kwa siku ya leo wafanyabiashara 2000 wamepatiwa vitambulisho[…]