Waziri Mkuu wa New Zealand Jacinda Ardern ameyashinikiza makampuni ya mitandao ya kijamii kutoa maelezo juu ya namna mshambuliaji alivyoweza kurusha moja kwa moja mitandaoni shambulizi lake kwa muda wa dakika 17, na video ya shambulizi hilo kuenea mitandaoni kwa saa kadhaa.

Aidha Waziri Mkuu huyo amesisitiza kuwa nchi hiyo inajipanga ndani ya siku kumi kuimarisha sheria ya umiliki wa bunduki ili kudhibiti matumizi holela ya silaha ambazo zimekuwa tishio kwa usalama wa jamii Leo kumekuwepo ulinzi mkali katika mji wa Christchurch nchini New Zealand, wakati shule na shughuli za kibiashara zikifunguliwa kwa mara ya kwanza tangu[…]

Watu Arobaini na tisa wameuawa na wengine zaidi ya ishirini wamejeruhiwa vibaya katika mashambulizi yaliyotokea katika misikiti miwili Christchurch nchini New Zealand.

Waziri mkuu wa New Zealand Jacinda Ardern ameelezea tukio hilo kuwa ni shambulizi la kigaidi na ni tukio baya kuikumba nchi hiyo. Maafisa wa polisi nchini humo wamesema wanaume watatu na mwanamke mmoja wanashikiliwa kuhusika na shambulizi hilo na kuonya kuna uwezekano wa kuwepo kwa watuhumiwa wengine zaidi. Waziri mkuu wa Australia Scott Morrison amesema[…]

Rais wa Marekani, Donald Trump ametangaza kusitisha mara moja safari za ndege za Boeing chapa 737 MAX 8, baada ya ndege kama hiyo ya Ethiopia kuanguka Jumapili iliyopita na kuwaua watu wote 157 waliokuwemo ndani.

Rais wa Marekani, Donald Trump ametangaza kusitisha mara moja safari za ndege za Boeing chapa 737 MAX 8, baada ya ndege kama hiyo ya Ethiopia kuanguka Jumapili iliyopita na kuwaua watu wote 157 waliokuwemo ndani. Akizungumza na waandishi habari katika Ikulu ya Marekani, Trump amesema amezipiga marufuku ndege hizo kuruka kutokana na kuongezeka kwa shinikizo[…]

Mamlaka ya kuratibu safari za anga za Marekani, FAA, imesema haitasimamisha safari za Ndege aina ya Boeing 737 Max, kufuatia ajali ya Ndege ya Shirika la ndege la Ethiopia iliyosababisha vifo vya watu 157.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, kaimu afisa mkuu wa mamlaka hiyo, Dan Elwell, alisema Jumanne kwamba uchunguzi uliofanywa kufikia sasa, haujabaini hitilafu yeyote katika mfumo wa Ndege hizo na kwa hivyo haoni haja ya kusitisha safari zake. Ajali hiyo imesababisha baadhi ya mashirika ya ndege ya nchi kadhaa kusitisha safari za ndege[…]

Shirika kuu la utangazaji la China CMG lajitahidi kufanya uvumbuzi na kujijenga kuwa chombo kikubwa cha habari cha aina mpya.

Shirika kuu la utangazaji la China CMG linajitahidi kutumia teknolojia mpya na kufanya uvumbuzi wa kuunganisha mbinu za kisasa za utangazaji kupitia majukwaa mbalimbali, ili kutangaza kwa ufanisi maamuzi ya Chama na maoni ya wajumbe kwenye Mikutano miwili inayoendelea kufanyika hapa Beijing. Wakati wa kuripoti Mikutano mwili ya mwaka huu, Shirika kuu la utangazaji la[…]

Teknolojia za kisasa kuleta mwelekeo mpya wa kuchanganywa kwa vyombo vya habari.

Vyombo vikuu vya habari vya China ikiwemo Shirika Kuu la Utangazaji la China vimetumia teknolojia ya kisasa katika kukusanya na kutangaza habari za mikutano ya Bunge la Umma na Baraza la Mashauriano ya kisiasa la China inayofanyika hapa Beijing. Wajumbe wanaohudhuria mikutano hiyo wamesema, teknolojia hizo zitaleta mwekeleo mpya wa kuchanganywa na kuendelezwa kwa vyombo[…]

Wanajeshi wa India na Pakistan wameshambulia vituo vya kijeshi na vijiji kwenye mpaka wao wenye shughuli nyingi za kijeshi wa jimbo linalogombaniwa la Kashmir, katika machafuko mapya licha ya nchi hizo mbili kuongeza juhudi za kutuliza mvutano.

Wanajeshi wa nchi hizo wametuhumiana kwa kuanzisha mashambulizi katika eneo hilo ambapo mpaka sasa hakuna habari zozote zilizotolewa mara kuhusiana hasara iliyotokea. Hofu imekuwa kubwa tangu ndege ya India iliporuka katika anga ya Pakistan wiki iliyopita ikifanya kile ambacho India ilisema ni shambulizi dhidi ya wanamgambo waliohusika na mlipuko wa bomu wa kujitoa mhanga Februari[…]