Teknolojia za kisasa kuleta mwelekeo mpya wa kuchanganywa kwa vyombo vya habari.

Vyombo vikuu vya habari vya China ikiwemo Shirika Kuu la Utangazaji la China vimetumia teknolojia ya kisasa katika kukusanya na kutangaza habari za mikutano ya Bunge la Umma na Baraza la Mashauriano ya kisiasa la China inayofanyika hapa Beijing. Wajumbe wanaohudhuria mikutano hiyo wamesema, teknolojia hizo zitaleta mwekeleo mpya wa kuchanganywa na kuendelezwa kwa vyombo[…]

Wanajeshi wa India na Pakistan wameshambulia vituo vya kijeshi na vijiji kwenye mpaka wao wenye shughuli nyingi za kijeshi wa jimbo linalogombaniwa la Kashmir, katika machafuko mapya licha ya nchi hizo mbili kuongeza juhudi za kutuliza mvutano.

Wanajeshi wa nchi hizo wametuhumiana kwa kuanzisha mashambulizi katika eneo hilo ambapo mpaka sasa hakuna habari zozote zilizotolewa mara kuhusiana hasara iliyotokea. Hofu imekuwa kubwa tangu ndege ya India iliporuka katika anga ya Pakistan wiki iliyopita ikifanya kile ambacho India ilisema ni shambulizi dhidi ya wanamgambo waliohusika na mlipuko wa bomu wa kujitoa mhanga Februari[…]

Kiongozi wa upinzani nchini Venezuela Juan Guaido amerejea leo nchini humo, baada ya ziara katika mataifa ya Amerika, na kushinikiza maandamano zaidi dhidi ya rais Nicolas Maduro.

Guaido ambaye alijiapisha kuwa rais wa watu na kuungwa mkono na mataifa ya Magharibi, yakiongozwa na Marekani, amepokelewa na maelfu ya wafuasi wake jijini Caracas. Kiongozi huyo amerejea nyumbani licha ya wasiwasi kuwa angekamatwa, baada ya kukiuka masharti ya Mahakama ya Juu, iliyokuwa imemzuia kutoka nje ya nchi hiyo. Hata hivyo Marekani imeionya serikali ya[…]

Rais wa Marekani Donald Trump amesema mkutano wa kilele kati yake na Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un mjini Hanoi, Vietnam umekamilika bila ya kufikiwa makubaliano kwa sababu hakuwa tayari kuiondolea Korea Kaskazini vikwazo.

Rais Trump amewaambia waandishi wa habari kuwa Korea Kaskazini ilitaka vikwazo vyote ilivyowekewa kuondolewa jambo ambalo Marekani haingeweza kulitekeleza. Hata hivyo Rais Trump amesisitiza kuwa bado wana uhusiano mzuri na Kiongozi wa Korea Kaskazini licha kupishana katika vipengele kadhaa katika mazungumzo yao. Awali, viongozi hao walikuwa wameonyesha matumaini ya kuimarisha mahusiano na kupiga hatua katika[…]

Mabingwa watetezi simba wameitandika bila huruma timu ya Lipuli FC kwa mabao 3-1 katika mchezo wa Ligi kuu Tanzania bara mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Samora Iringa.

Simba ndio waliokuwa wa kwanza kuliona lango la Lipuli FC kuptia kiungo wao machchari Cloutus Chama ambaye alikuwa kwenye kiwango bora kwenye mchezo huo ambao ulikuwa wa ufundi mkali. Bao hilo liliwaamusha Lipuli ambao walifanya mashambulizi ya hapa na pale na kufanikiwa kusawazisha bao hilo kupitia mshambuliji wao Paul Nonga aliyefunga kwa shuti kali baada[…]

Zoezi la kukusanya picha kwa ajili ya maadhimisho ya “miaka 55 ya uhusiano wa kibalozi kati ya China na Tanzania”.

Mwaka huu China na Tanzania zinaadhimisha miaka 55 tangu zianzishe uhusiano wa kibalozi. Ili kuadhimisha na kudumisha urafiki wa jadi kati ya nchi hizi mbili, Idhaa ya Kiswahili ya Shirika Kuu la Utangazaji la China imeandaa shindano la kukusanya picha kwa ajili ya maadhimisho hayo. A。Tunachohitaji Picha zinazoonesha urafiki kati ya Tanzania na China, zinazoonesha[…]

Serikali ya Yemen na wawakilishi wa wanamgambo wa kishia-Houthi wamekubaliana kuhusu awamu ya kwanza ya kuwaondoa wanajeshi kutoka mji wa bandari wa Hodeida.

Serikali ya Yemen na wawakilishi wa wanamgambo wa kishia-Houthi wamekubaliana kuhusu awamu ya kwanza ya kuwaondoa wanajeshi kutoka mji wa bandari wa Hodeida na katika bandari za Salif na Ras Isa ambapo Umoja wa mataifa umesema hayo ni makubaliano muhimu yaliyofikiwa. Bandari ya Hodeida ni muhimu kwa kuwa huko ndiko inakofikia misaada ya jumuia ya[…]