Serikali yaingilia kati Bei ya Maziwa.

Serikali imeamua kuingilia kati bei ndogo ya ununuzi wa maziwa, inayotolewa na viwanda vya kusindika maziwa nchini, na hivyo kusababisha wazalishaji wa maziwa kushindwa kumudu gharama kubwa za uzalishaji. Uamuzi huo wa serikali umetangazwa jijini Dodoma na Waziri wa Mifugo na Uvuvi BW. Luaga Mpina, wakati wa Maonesho ya Ng’ombe Bora wa Tanzania, ambapo jumla[…]

Watakiwa kuacha kuigana kubuni Miradi.

Serikali imewataka viongozi wa halmashauri zote nchini, kuacha kuigana katika uanzishaji wa miradi ya vitega uchumi katika maeneo yao, na badala yake wabuni miradi itakayoiwezesha halmashauri hizo kujitegemea kimapato. Ushauri huo umetolewa katika jiji la Dodoma kwenye Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali[…]

TANESCO wawezesha Wabunifu wa Umeme wa Maji Njombe.

Wabunifu wawili, John Fute maarufu Mzee Pwagu kutoka kijiji cha Msete na Lainery Ngailo kutoka kijiji cha Lugenge mkoani Njombe ambao wamejizolea umaarufu kutokana na ubunifu wa kuzalisha umeme wa maji kwa kutega kutoka kwenye vyanzo vya mito, wamewezeshwa na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) shilingi milioni 15 kila mmoja ili ziwasaidie kuboresha miundombinu ya[…]

Serikali yaendelea Kuboresha Mazingira ya Biashara.

Serikali imechukua hatua mbalimbali za kuboresha mazingira ya uwekezaji na kufanya biashara hapa nchini, ikiwa ni pamoja na kuimarisha zaidi sekta binafsi ili iweze kutoa mchango wake unaohitajika kwa uchumi wa taifa. Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji Angella Kairuki amebainisha hayo jijini Dar es salaam wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa[…]

Waziri wa Kilimo aingilia kati kero ya ununuzi wa Pamba.

Baada ya Wakulima wa Pamba Mkoani Simiyu, kulalamika kwamba Pamba waliyolima na kuvuna haijanunuliwa, Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga amewataka wanunuzi waliopewa Leseni na Bodi ya Pamba nchini, kuanza kununua Pamba hiyo, wakati Serikali ikitafuta ufumbuzi wa kasoro ndogo zilizojitokeza tatika msimu wa mwaka 2018/2019. Siku chach baada ya wakulima wa pamba mkoani Simiyu, kuzungumza[…]