Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe amesema wizara hiyo inaendesha Kampeni ya kutoa elimu nchi nzima kwa vijana ili vijana hao waweze kukuza vipaji vyao pamoja na kuwa na weledi katika utengenezaji wa picha za filamu.

Dkt. Mwakyembe ameyasema hayo katika Mji mdogo wa Nduguti,wilayani Mkalama baada ya kupokea taarifa ya wilaya hiyo iliyoonyesha jitihada za kulikarabati jengo la Boma la Mjerumani na kubaini pia kuwa wilaya ya Mkalala bado ipo nyuma katika masuala ya utengenezaji wa picha za filamu na ndipo akatoa ahadi kwa wana – Mkalama. Aidha Dkt. Mwakyembe[…]

Kamati ya Saa 72 inayosimamia Ligi Kuu Tanzania Bara yailima faini ya milioni Sita Yanga pamoja na Kutoa Onyo kali kwa Makocha wa Vilabu Vinavyoshiriki Ligi Kuu Bara kwa utovu wa Nidhamu.

Akizungumza jijini Dar es Salaam mtendaji mkuu wa bodi ya ligi Boniface Wambura amewataka makocha ambao wanashambulia waamuzi wapeleke ushahidi ndani ya shirikisho la soka TFF kwaajili ya hatua zichukuliwe na vyombo vinavyoongoza shirikisho hilo. Aidha Wambura ameainisha adhabu kwa timu za Simba,Yanga na Azam Fc ambazo zilikiuka utaratibu wa kisheria kwa kutotumia milango rasmi[…]

Jijini Dar es Salaam katika kuadhimisha siku ya radio duniani leo baadhi ya wananchi wameelezea umuhimu wa chombo hicho katika kufikisha ujumbe na taarifa mbalimbali muhimu kwa umma kwa haraka.

Jijini Dar es Salaam katika kuadhimisha siku ya radio duniani leo baadhi ya wananchi wameelezea umuhimu wa chombo hicho katika kufikisha ujumbe na taarifa mbalimbali muhimu kwa umma kwa haraka na hivyo kuchochea maendeleo ya kijami na kiuchumi. Channel Ten imezungumza na baadhi ya wananchi jijini Dar es Salaam ambao wamesema, kutokana na kukua kwa[…]

Wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano ya kimataifa ngazi ya klabu, Timu ya Simba ya DSM leo watakuwa Uwanja wa Taifa wakitafuta pointi muhimu mbele ya timu ya Al Ahly ya Misri.

Mchezo huo wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika ni wa mzunguko wa nne na mpaka sasa hakuna timu ambayo ina uhakika wa kwenda robo fainali kwenye kundi lao la D. Simba ipo Kundi D ikiwa na timu za Al Ahly iliyo kileleni na pointi saba, AS Vita ya CONGO DRC yenyewe ni[…]

Aliyekuwa Makamu wa Rais wa TFF, Michael Wambura amesomewa mashitaka 17 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini DSM ikiwemo utakatishaji fedha wa Mil.75.

Katika kesi hiyo Wambura anakabiliwa na shtaka moja la kughushi, Shtaka moja la kutoa nyaraka za uongo, mashtaka 13 ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na mashtaka mawili ya kutakatisha fedha. Akisoma hati ya mashtaka wakili wa serikali George Barasa akisaidiana na Moza Kasubi pamoja na Imani Mitumezizi mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Kelvin[…]

Shirika la Reli Tanzania limesema kuwa milango bado ipo wazi kwa makundi mbalimbali kuutembelea mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa ya SGR inayojengwa kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza kwa lengo la kujifunza kama walivyofanya wasanii mbalimbali nchini.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa TRC Masanja Kungu Kadogosa mara baada ya kupokea wasanii,wanamichezo na washereheshaji zaidi ya 300 waliotembela mradi wam Ujenzi wa Reli hiyo ya kisasa. Wasanii hao walitumia usafiri wa treni ya delux na kushuhudia ujenzi wa Reli hiyo wakiwa ndani ya treni hiyo ambapo pia walikuwa wakishuka na kujionea[…]

Jeshi la Polisi la Dorset limethibitisha kwamba Mwili ulioopolewa kutoka kwenye mabaki ya ndege iliyoanguka ni wa mchezaji soka wa timu ya Cardiff City, Emiliano Sala.

Sala, aliyekuwa na umri wa miaka 28, alikuwa akisafiri kwenda Cardiff katika ndege ambayo,rubani wake alikuwa ni David Ibbotson, ilipotea mnamo Januri 12. Kwa mujibu wa BBC. Mwili wake ulipatikana Jumatano baada ya kugunduliwa kwa mabaki ya ndege hiyo Jumapili asubuhi. Polisi ya Dorset imethibitisha utambulisho wake Alhamisi usiku katika taarifa yake, kikosi hicho kimesema[…]

Michuano ya kombe la SportPesa inayoshirikisha timu nane za Tanzania na Kenya mwaka huu itaonyeshwa kupitia DSTV.

Michuano ya kombe la SportPesa inayoshirikisha timu nane za Tanzania na Kenya mwaka huu itaonyeshwa kupitia Kampuni ya Utangazaji ya Multichoice Tanzania, kupitia king’amuzi chake cha DSTV. Makubaliano ya ushirikiano huo yametangazwa mbele ya waandishi wa habari jijini DSM, na viongozi wa pande hizo mbili, Multichoice Tanzania ikiwakilishwa na Mkurugenzi wake Mtendaji Jacqueline Woiso na[…]

Klabu ya simba imefanikiwa kuichapa klabu ya Js saoura kutoka Algeria katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Katika mchezo wa leo Uliotazamwa na Waziri mkuu Mh kassim majaliwa pamoja na Naibu spika wa bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania Tulia Ackson Mwansasu,Klabu ya simba Imepata ushindi wa Magoli 3-0 dhidi ya Js saoura. Goli la kwanza liliwekwa nyavuni katika kipindi cha kwnza na Mshambuliji wa Simba Emmanuel Okwi na magoli mawili[…]

Wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano ya kimataifa Simba na Mtibwa Sugar wameshindwa kutamba kwenye viwanja vya ugenini baada ya kupoteza michezo yao hii leo.

Simba ya Dar es Salaam inayoshiriki Ligi ya Mabingwa Afrika imeshindwa kutamba mbele ya Nkana Red Devils ya Zambia, baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-1, wakati Mtibwa Sugar wametandikwa mabao 3-0 na KCCA. Bao la kufutia machozi la Simba limefungwa na Nahodha John Boko kwa njia ya penalti, baada ya Meddie Kagere kufanyiwa madhambi[…]