Wanafunzi zaidi ya mia saba na waalimu wajisaidia vichakani kutokana na shule kukosa vyoo mkoani Tabora

WANAFUNZI wa shule ya msingi Budushi iliopo kata ya Budushi tarafa ya Puge wilaya ya Nzega mkoani Tabora wanajisaidia vichakani kutokana na shule hiyo kukosa vyoo vya wananfunzi na walimu. Wakizungumza na Channel ten baadhi ya wanafunzi hao wameeleza changamoto ya ukosekanaji wa vyoo katika shule ya msingi Budushi hivyo wanaiomba serikali iweze kutatua changamoto[…]

Mashamba ya bangi yateketezwa kwa moto wilayani Kaliua

Zaidi ya hekari 30 za bangi zimeteketezwa kwa moto katika eneo la hifadhi ya Igombe Nkulu wilayani Kaliua mkoani Tabora katika jitihada za kupambana na dawa za kulevya. Katika oparesheni hiyo iliyoanza kutekelezwa wilayani kaliua makamanda wa vikosi mbali mbali vya ulinzi na usalama wa mkoa huu wamesema wako tayari kutekeleza agizo la amiri jeshgi[…]

Serikali yasema hakuna njaa nchini Tathimini ya hali ya chakula katika Halmashauri 55 yaendelea

Serikali imesema hakuna njaa nchini, na kwa sasa hali ya chakula inaridhisha licha ya eneo kubwa la nchi kukosa mvua za msimu wa vuli ambazo zimesababisha ukame kwa baadhi ya maeneo. Kwa sasa Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi kwa ushirikiano na ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI, Shirika la Chakula Duniani, Taasisi ya Chakula na[…]

Tishio la Njaa Kwimba, Wananchi wawasilisha kilio serikalini

Wakati tishio la njaa likiendelea kutikisa katika maeneo mbalimbali nchini kutokana na ukame, wakazi wa Kijiji cha Manawa wilayani Kwimba mkoani Mwanza, wamelazimika kuzuia msafara wa mkuu wa mkoa huo John Mongela, ili kuwasilisha kilio cha njaa inayowakabili. Kutokana na kilio hicho kilichosababishwa na ukosefu wa Mvua, wakazi hao wamelazimika kubeba mabua ya Mahindi yaliyokauka,[…]

Vladmiri Putin Aliamuru udukuzi dhidi ya Hillary Clinton

Urusi imepinga shutuma kuwa Rais wa nchi hiyo Vladmir Putin,aliamuru ufanyike udukuzi,dhidi ya Hillary Clinton na Chama chake cha Democratic,kumsaidia Donald Trump,kushinda uchaguzi mkuu wa nchi hiyo. Andrey Klimov,ambaye ni makamu mwenyekiti wa Seneti inayoshughulika na uhusiano wa kimataifa,amesema,Urusi ni tishio na imekuwa ikisakamwa kwa maneno mabaya huku Ikulu ya nchi hiyo maarufu kama Klemlin,ikifananishwa[…]

Tabia ya wizi imeibuka mabasi yaendayo haraka jijini Dar es salaam

Abiria wanaotumia usafiri wa mabasi yaendayo haraka jijini Dar es salaam wameomba waendesha mradi UDA-RT kuimarisha ulinzi katika vituo vya mabasi hayo kutokana na kuibuka kwa tabia ya wizi katika vituo hivyo jambo ambalo hapo awali halikuwepo. Wakizungumza na Channel Ten abiria hao wamesema wanadhani tatizo hilo limeibuka katika kipindi hiki kutokana na kusitishwa kwa[…]

Rais Magufuli, leo amemuapisha Kamishna wa Polisi Diwani Athuman Msuya kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo amemuapisha Kamishna wa Polisi Diwani Athuman Msuya kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera. Hafla ya kuapishwa kwa Kamishna Diwani Athuman Msuya imefanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Jaji Mkuu wa Tanzania Mohamed Chande Othman, Waziri wa[…]