Watu saba wamefariki dunia na wengine watatu wamejeruhiwa kwenye ajali ya barabarani iliyotokea barabara kuu ya Dodoma Morogoro eneo mbande wilayani kongwa mkoani Dodoma.

Ajali hiyo imetokea usiku wa kuamkia leo nakuhusisha magari matatu, ambapo mawili kati yake ni magari ya serikali yenye namba za usajili STL 6250 mali ya ofisi ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali na lingine ni SU 41173 mali ya mfuko wa hifadhi za jamii wa PSSSF na lori la mizigo aina ya mitsubish fuso.

Kwa mujibu wa majeruhi wanadai ajali hiyo imetokea baada ya gari la Ofisi ya CAG likitokea wilayani Chato kuligonga lori aina ya fuso ambalo lilikuwa limeharibika katikati ya barabara bila kuweka tahadhari na kisha kupoteza mwelekeo na kugongana uso kwa uso na gari mali ya PSSSF lililokuwa likitokea jijini Dar es salaam kuelekea Dodoma.

Ndugu wa marehemu ambao wamefika hosipitali ya rufaa ya mkoa wa dodoma ambako miili imehifadhiwa wanasema marehemu walikuwa wakitoka wilayani chato kwenye msiba wa mama wa Naibu CAG BENJAMINI MASHAURI MAGAYI na si watumishi wa taasisi.

Katibu mkuu wizara ya mambo ya ndani RAMADHANI KAILIMA anasema imefika wakati serikali kuzuia matumizi ya magari yake nyakati za usiku ili kutoa muda kwa madereva kupumzika huku kaimu mganga mkuu wa hosipitali ya rufaa ya dodoma akithibitisha kupokea miili ya marehemu na majeruhi.

Tazama Video hapa Chini;

Comments

comments