EWURA imeanzisha mfumo wa ujenzi wa vituo vya mafuta vyenye masharti nafuu kwenye maeneo ya vijijini ili kukabiliana na biashara ya kuuza mafuta kwenye vifaa visivyoruhusiwa kisheria.

MAMLAKA ya Udhib iti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imeanzisha mfumo wa ujenzi wa vituo vya mafuta nyenye masharti nafuu kwenye maeneo ya vijijini ili kukabiliana na biashara ya kuuza mafuta kwenye vifaa visivyoruhusiwa kisheria.

MENEJA Mawasiliano na Mahusiano wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA),BWANA TAITUS KAGUO ameyasema hayo kwenye semina ya siku mbili ya kutambulisha ofisi za EWURA Kanda ya kati iliyopo Mkoani Dodoma inayoshughulikia mikoa ya Dodoma,Singida,Tabora na Iringa iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Chuo cha elimu ya ufundi stadi (VETA) Mkoa wa Singida.

AMESEMA BWANA KAGUO kwamba changamoto ya baadhi ya wananchi kuuza mafuta ya petroli kwenye vifaa visivyo rasmi inatokana na uingizwaji wa vyombo vya usafiri aina ya pikipiki inayoweza kutumia mafuta kidogo kwa muda wa siku nzima.

MENEJA wa EWURA Kanda ya kati,ENG,NORBERT KYOZA amebainisha kwamba bado kuna matatizo kidogo kwenye biashara ya mafuta hayo na kimsingi endapo wakiachia kila mmoja akafanya biashara hiyo anavyotaka,madhara yatakuja kwa watu wote.

NAO baadhi ya wauzaji wa mitungi ya gesi na mafuta aina ya petroli,BI TATU IDDI pamoja na BI TEDDY DULE wakaelezea changamoto zinazowakabili na kutoa ushauri kwa mamlaka zinazosimamia biashara hizo.

Comments

comments