Hatimaye Marekani imerejesha Ubalozi wake nchini Somalia, kwa mara ya kwanza baada karibu miaka 30.

Wizara ya Mambo ya nje imesema, hatua hii imefikiwa, kutokana na juhudi za kiusalama na kisiasa zilizopigwa katika taifa hilo.

Akizungumza kuhusu kufunguliwa kwa ubalozi huo, Waziri Msaidizi wa mambo ya nje wa Marekani, Wendy Sherman anayehusika na maswala ya kisiasa amesema kufunguliwa kwa ubalozi huo pia ni ishara ya kuwa Marekani ina imani yakwamba Somalia, ambayo imeharibiwa na vita, itaweza kupata utulivu na kufikia malengo yake.

Balozi wa Marekani, ambaye makazi yake yamekuwa jijini Nairobi nchini Kenya, anatarajiwa kuhamia mjini Mogadishu hivi karibuni.

Marekani ilifunga Ubalozi wake nchini Soamlia mwaka 1991, baada ya kuzuka kwa vita kati ya waasi na wanajeshi wa serikali.

Comments

comments