Rais wa Marekani Donald Trump aishangaza dunia katika tukio la ibada ya mazishi ya kitaifa ya Rais wa 41 wa nchi hiyo George Hubert Walker Bush,jijini Washington.

Rais wa Marekani Donald Trump,jana ameishangaza dunia kufuatia kitendo chake kisichofaa wakati wa tukio la ibada ya mazishi ya kitaifa ya Rais wa 41 wa nchi hiyo George Hubert Walker Bush,jijini Washington.

Trump akiwa ameongozana na mke wake Melania Trump,aliingia katika kanisa kuu la nchi hiyo na kwenda mahala alipopangiwa kukaa yeye na marais wa zamani wa nchi hiyo.Jambo lililowakera wengi na kila mmoja kutoa tafsiri yake,ni kitendo chake cha kumpuuza Rais wa zamani wa nchi hiyo Bill Clinton na mke wake Hillary.

Kabla ya Trump kuingia mahala hapo,kufuatia mpangilio wa ukaaji,Bill Clinton,alikuwa akizungumza kwa pamoja na Barack na Michelle Obama,wakati Hilary Clinton,alikuwa akizungumza na Rais wa 39 wa nchi hiyo Jimmy Carter.

Alipoingia Trump,mke wake kwa heshima,aliwapa mikono Barack na Michelle Obama pamoja na Bill Clinton,na kumpungia mkono Hilary Clinton.Donald Trump,alianza kuvua jaketi lake na kuliweka kwenye kiti ndipo akaenda kumsalimia mtangulizi wale Barack Obama na Michelle.

Lakini akajifanya hajaiona na kutoisalimia familia ya Clinton,Hillary Clinton,alikuwa hasimu wake katika uchaguzi mkuu wa nchi hiyo mwaka 2016.

Comments

comments