IGP Sirro aunda Kamati ya Kukusanya Vielelezo.

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro ameunda Kamati itakayoongozwa na Maafisa tisa watakaozunguka na kupita vituo vyote vya Polisi nchi nzima kuhakikisha vielelezo vyote vinaondolewa maeneo hayo pamoja na kuhakikisha vinafikishwa Mahakamani.

IGP Sirro amesema hayo jijini Dar Es Salaam jana alipokutana na Makamanda wa Polisi kutoka mikoa thelathini na mitano kote Nchini, ambapo pia amewaagiza kwenda kusimamia sheria, kanuni na taratibu za nchi ikiwa ni pamoja na kuwachukulia hatua kali za kisheria Maafisa na Askari wanaokwenda kinyume na mwenendo mwema wa Jeshi la Polisi.

Aidha, IGP Sirro amewataka Makamanda wa Polisi kote nchini kuhakikisha wanatoa huduma bora kwa wananchi ikiwemo kupunguza mlundikano wa kesi mbalimbali zilizoripotiwa katika vituo vya Polisi.

Comments

comments