Jijini Dar es Salaam katika kuadhimisha siku ya radio duniani leo baadhi ya wananchi wameelezea umuhimu wa chombo hicho katika kufikisha ujumbe na taarifa mbalimbali muhimu kwa umma kwa haraka.

Jijini Dar es Salaam katika kuadhimisha siku ya radio duniani leo baadhi ya wananchi wameelezea umuhimu wa chombo hicho katika kufikisha ujumbe na taarifa mbalimbali muhimu kwa umma kwa haraka na hivyo kuchochea maendeleo ya kijami na kiuchumi.

Channel Ten imezungumza na baadhi ya wananchi jijini Dar es Salaam ambao wamesema, kutokana na kukua kwa teknolojia, chombo kama radio kimekuwa msaada mkubwa kwa wao kupata habari kwa haraka na kwa wakati mahala walipo bila vikwazo hivyo kuwajengea ufahamu wa kutosha wa masuala mbalimbali ya kijamii, kama vile Afya, Elimu, na hata Maendeleo kuhusu Taifa na dunia kwa ujumla.

Aidha wanachi hao wameipongeza serikali kwa kutoa uhuru mpana wa kuwepo kwa radio mbalimbali ambazo zimekuwa zikiwahudumia wananchi hususan kwa kuwahabarisha, kuwaburudisha pamoja na kuwaelimisha kuhusu masuala mbalimbali ya ndani na nje ya nchi.

Kampuni ya Afrika Media Group, inayomiliki kituo cha Channel Ten pia inamiliki Radio Magic FM ambayo tangu kuanzishwa kwake imevuta wasikilizaji wengi. Baadhi ya watangazaji wa Radio Magic wamezungumzia maadhimisho ya Siku ya Radio duniani.

Shirika la kimataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) lilianzisha Siku ya Radio Duniani mwaka 2012 mara baada ya Baraza Kuu la UNESCO kutambua umuhimu wake na mwaka uliofuata Umoja wa Mataifa ukatambua Siku ya Radio duniani ambayo huadimishwa kila Februari.13 kauli mbiu mwaka huu ikiwa ni Mazungumzo, kuvumiliana na Amani.

Comments

comments