Jumuiya ya wanawake wa chama cha Mapinduzi CCM mkoani Pwani -UWT-wameadhimisha Siku ya Wanawake duniani kwa kupaka rangi mnara wa bibi Titi Mohammed ikiwa ni ishara ya kumuenzi mwasisi huyo wa CCM kwa upande wa wanawake nchini.

Katika kuelekea siku ya wanawake duniani wanawake wa mkoa wa Pwani CCM wameazimisha Siku hiyo katika kijiji cha mkongo kata ya mkongo wilaya Rufiji ambapo pamoja Na shughuli nyingine wametumia fursa hiyo kungarisha mnara huo uliojengwa….ikiwa ni ishara ya kumuenzi mwanasiasa hiyo mkongwe aliyekuwa miungoni mwa viongozi wa awamu ya kwanza waliopigania Uhuru wa nchi.

Katika maadhimisho hayo mwenyekiti wa UWT mkoa wa Pwani Farida Mgome alitumia fursa hiyo kueleezea mambo mbalimbali aliyoyafanya bibi Titi Mohammed.

Kijiji cha mkongo kimekuwa na historia mbalimbali ikiwa in pamoja na kuwa kijiji cha kwanza kutengwa katika opereshen vijiji mwaka 1974 lakini pia mkutano mkuu wa halmashauri kuu ya Taifa ya TANU ulifanyika katika kijiji hicho.

Comments

comments