Kampuni ya Mawasiliano ya Simu za Mkononi Halotel imetiliana saini ya makubaliano na kampuni ya michezo ya kubahatisha na kubashiri ya Biko lengo likiwa kuwawezesha wateja wanaotumia mtandao huo kupitia Halopesa kuvuna mamilioni ya fedha

Kampuni ya Mawasiliano ya Simu za Mkononi Halotel imetiliana saini ya makubaliano na kampuni ya michezo ya kubahatisha na kubashiri ya Biko lengo likiwa kuwawezesha wateja wanaotumia mtandao huo kupitia halopesa kuvuna mamilioni ya fedha kutoka Biko ili kujiongezea kipato na kuboresha maisha yao.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam mkuu wa kitengo cha mawasiliano Halotel Mhina Semwenda amesema makubaliano hayo yatasaidia kwa kiasi kikubwa wateja wa mijini na vijijini kushiriki kwenye mchezo wa kubahatisha na kubashiri ambapo wateja hao walikuwa hawapati fursa ya kucheza mchezo huo.

Comments

comments