Kamati ya Saa 72 inayosimamia Ligi Kuu Tanzania Bara yailima faini ya milioni Sita Yanga pamoja na Kutoa Onyo kali kwa Makocha wa Vilabu Vinavyoshiriki Ligi Kuu Bara kwa utovu wa Nidhamu.

Akizungumza jijini Dar es Salaam mtendaji mkuu wa bodi ya ligi Boniface Wambura amewataka makocha ambao wanashambulia waamuzi wapeleke ushahidi ndani ya shirikisho la soka TFF kwaajili ya hatua zichukuliwe na vyombo vinavyoongoza shirikisho hilo.

Aidha Wambura ameainisha adhabu kwa timu za Simba,Yanga na Azam Fc ambazo zilikiuka utaratibu wa kisheria kwa kutotumia milango rasmi wakati wa kuingia uwanjani pamoja na vyumba vya ukaguzi kabla ya mchezo.

Adhabu nyengine ni kocha wa timu ya Alliance FC Malale Hamsini amefungiwa mechi 2 na faini ya laki 5,kocha wa mwadui Ally Bimuzungu amelimwa faini ya laki 2 pamoja na kocha wa Mbeya City Ramadhan Swazilimo amepewa onyo kali kwa kutoa maelekezo akiwa jukwaani.

Comments

comments