Kampuni ya Reli Tanzania TRL leo imezindua Treni maalum ya kubeba mizigo

1 (1)

Kwa mara nyingine Kampuni ya Reli Tanzania TRL leo imezindua Treni maalum ya kubeba mizigo(BLOCK TRAIN)Itakayokuwa inatumika kusafirisha mizigo mbalimbali iikiwemo mizigo ya Shirika la Mpango wa Chakula Duniani WFP kutoka bandari ya Dar es salaam na kuelekea ghala kuu ya Chakula ya Shirika hilo iliyopo Kizota Mkoani Dodoma.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo ya uzinduzi uliofanyika jijini Dar es salaam Mkurugenzi Mtendaji wa TRL Masanja Kadogosa amesema lengo la uanzishwaji wa Usafirishwaji wa Shehena kwa kutumia usafiri wa Reli ni kuhudumia wateja kwa muda unaoridhisha hali itakayowezesha kuongeza imani ya wateja sanjari na Kuongeza kipato ndani ya Shirika hilo.

Kwa Upande wake Mwakilishi Mkazi kutoka Shirika la Chakula Duniani WFP Michael Dunford amesema huo ni mwanzo wa Ushirikiano Mzuri baina ya Shirika hilo na Serikali ya Tanzania katika sekta ya Usafirishaji huku akiisifu Serikali ya Tanzania katika kuboresha sekta ya Usafirishaji na kuongeza kuwa itashirikiana na TRL katika kusafirisha Shehena mbalimbali za mizigo ikiwemo Chakula kwa ajili ya kupeleka maeneo mbalimbali.

Comments

comments