Waziri Joseph Kakunda amewataka wale wote walionunua korosho kwa wakulima maarufu kama kangomba warudishe korosho hizo kwa wakulima kwani serikali haitawafumbia macho wafanyabiashara hao

Waziri wa viwanda,biashara na uwekezaji Joseph Kakunda amewataka wale wote walionunua korosho kwa wakulima maarufu kama kangomba warudishe korosho hizo kwa wakulima kwani serikali haitawafumbia macho wafanyabiashara hao bali itaendelea kuhakiki korosho mpaka mashamba yao.

Waziri Kakunda ametoa kauli hiyo jijini dar es salaam akiwa katika viwanja vya maonyesho ya kimataifa mwalimu nyerere maarufu sabasaba ikiwa ni siku ya kwanza ya maonyesho ya viwanda na kusisitiza kuwa nia ya serikali ni kuhakikisha wakulima wananufaika kilimo na kueleza kuwa kangomba wananunua kilo moja ya korosho kwa shilingi 600 huku bei elekezi ikiwa ni 3300.

Akizungumzia maonyesho hayo ya tatu Waziri Kakunda amesema yanawakutanisha wenye viwanda, wafanyabiashara na watafiti hivyo watapata fursa ya kujadili changamoto zinazokwaza wawekezaji na kuzitafutia ufumbuzi kupitia kliniki ya biashara ambayo ipo katika viwanja hivyo na kuwataka watanzania kutumia fursa hiyo kubadilishana uzoefu na kutafuta masoko pamoja na kupata vitambulisho vya taifa.

Maonyesho hayo yenye kauli mbiu isemeyo Tanzania sasa tanajenga viwanda yanatarajiwa kufunguliwa rasmi kesho na kuhitimishwa desemba 9 mwaka huu.

Comments

comments