Katibu Mkuu Dkt. Bashiru Ally awajulia hali Majeruhi wa ajali ya Moto.

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Bashiru Ally ameipongeza serikali ya awamu ya tano katika kuendelea kuwekeza katika miundombinu wezeshi ikiwemo sekta ya elimu na sekta ya afya katika kusaidia nchi kuondokana na utegemezi wa misaada na kujitengemea wenyewe.

Dkt. Bashiru amesema hayo wakati wa ziara yake mkoani Morogoro na kuwajulia hali majeruhi wa ajali ya Moto ambapo amesema kuwa kitendo cha majeruhi wa ajali ya hiyo kuishia kutibiwa katika hospitali za ndani ni kipimo cha nchi kuwa na uwezo wa kujitengemea ikiwa ni matokeo ya uwekezaji mkubwa unaoendelea kufanywa na serikali ya awamu ya tano chini ya rais Dkt. John Magufuli.

Ziara ya Katibu mkuu wa ccm mkoani morogoro imelenga kutembelea na kutoa pole Majeruhi wa ajali hiyo ya Moto ambapo akiwa mkoani hapa mkuu wa mkoa wa Morogoro Dkt Kebwe akatoa taarifa ya ongezeko la vifo vya majeruhi waliolazwa katika hospitali ya taifa ya Muhimbili( na kufikia idadi ya watu 82 huku majeruhi 16 waliolazwa hospitali ya mkoa wa Morogoro wakiendelea vizuri na matibabu).

Comments

comments