Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Temeke jijini Dsm limetangaza kuwachukulia hatua kali ikiwemo kuwafungulia Mashitaka Wazazi au Walezi ambao watoto wao wamefanyiwa Ukatili na wao wakanyamaza na kulipwa fedha na wahalifu

Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Temeke jijini Dsm limetangaza kuwachukulia hatua kali ikiwemo kuwafungulia Mashitaka Wazazi au Walezi ambao watoto wao wamefanyiwa Ukatili ikiwemo kubakwa,kulawitiwa,kupewa Ujauzito kwa Wasichana au kuteswa na baadae wazazi au walezi kuingia Makubaliano na Mtuhumiwa kwa kulipwa fedha ili mtuhumiwa asifikishwe katika vyombo vya Sheria.

Akizungumza wakati wa Uzinduzi wa maadhimisho ya siku 16 ya Kupinga Ukatili dhidi ya wanawake na watoto katika wilaya ya Temeke,Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Temeke Emmanuel Lukula amesema baadhi ya wazazi au walezi ambao watoto wao wamefanyiwa Ukatili wamekuwa wakipeleka taarifa polisi lakini baadae polisi inapochukua hatua wahusika huingia makubaliano ya kulipana fedha na kusababisha kesi hizo kuishia hewani.

Mkuu wa wilaya ya Kigamboni Sarah Msafiri ambaye alikuwa Mgeni rasmi akizungumza ktk maadhimisho hayo amesema Pamoja na vitendo vya Ubakaji na Ulawiti lakini matukio mengi wananchi wameshindwa kwenda kutoa Ushahidi mahakamani na wengine kuingia Makubaliano ya fidia na baadae watuhumiwa kuwa huru na kuendelea na vitendo hivyo.

Comments

comments