Mgomo kwa baadhi ya wasafirishaji wa zao la Korosho kutoka katika vyama vya msingi kwenda maghala makuu, Mkuu wa mkoa wa Lindi Godfrey Zambi ameitisha kikao kazi

Wakati Wizara ya Kilimo ikiongeza Wataalamu wa Uhakiki wa Wakulima wa Korosho katika mikoa ya Mtwara, Lindi na Ruvuma, ikiwa ni jitihada za kuharakisha uhakiki kwa ajili ya malipo ya wakulima, imebainika kuwepo mgomo kwa baadhi ya wasafirishaji wa zao hilo kutoka katika vyama vya msingi kwenda maghala makuu.

Kufuatia changamoto mbalimbali za ukusanyaji na uuzaji wa korosho msimu huu, ikiwemo changamoto ya wakulima wengi kutolipwa kwa wakati, huku korosho zingine zikishindwa kusafirishwa baada ya watoa huduma za usafiri kuanza kugoma kutokana na kutojua hatma ya malipo yao.

Pamoja na changamoto hizo, Mkuu wa mkoa wa Lindi Godfrey Zambi ameitisha kikao kazi kujadili hali hiyo, huku tayari Shs bilioni 35 zikiwa tayari zimekwishalipwa kwa wakulima wa korosho.

Comments

comments