Kufuatia taharuki iliyowapata wakazi wa jiji la Arusha kwa takribani wiki moja na nusu sasa baada ya baadhi yao kulalamikia kusumbuliwa na magonjwa ya tumbo, Mkuu wa mkoa huo Mrisho Gambo ameingilia kati na kuagiza wataalam wa afya kufanya uchunguzi wa kina kubaini chanzo cha malalamiko hayo ili hatua stahiki zichukuliwe.

Gambo ambae amelazimika kutembelea makazi ya wananchi katika eneo la Pangani ya chini na daraja mbili jijini humo yanayodaiwa kukumbwa na mlipuko huo na kuzungumza na wananchi wa maeneo hayo,ambapo yeye binafsi na viongozi wengine wakaamua kujiridhisha usalama wa maji hayo kwa kuyanywa.

Hata hivyo kaimu mganga mkuu wa hospitali ya mkoa ya mountmeru Dkt. Omar Chande amesema kuwa baada ya kusikia taarifa za mlipuko huo amekiri kupokea wagonjwa 310 katika zahanati na vituo vya afya wakisumbuliwa na magonjwa ya tumbo ambao walitibiwa na kuondoka.

Baada ya ziara yake Gambo amewataka wananchi wa jiji la Arusha kuwa watulivu wakati serikali ikishughulikia haraka tatizo hilo kupitia wataalam wa afya.

Takribani wiki moja na nusu sasa kumekuwa na taarifa mbalimbali zikienea katika mitandao ya kijamii zikidai kuwa zoezi la ukarabati miundombinu ya mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira limesababisha kuchafuka kwa majisafi na majitaka hivyo kusababisha mlipuko wa ugonjwa wa kuhara.

Comments

comments