Kufuatia kifo cha rais wa zamani wa Marekani wa 41 George Herbert Walker Bush, viongozi wa mataifa wameendelea kutuma salamu za rambirambi na kumkumbuka mwanasiasa huyo wakiongozwa na Rais wa sasa wa Marekani Donald Trump

Trump amemsifu Bush Senior kama alivyofahamika zaidi kwa uhalisia wake wa ucheshi na kujitolea kwake kudumisha amani, kwa familia na taifa kwa ujumla.

George Bush Senior aliyefariki na miaka 94, alikuwa rais kati ya mwaka 1989 na 1993 baada ya kuongoza kwa mihula miwili kama makamu wa rais chini ya Rais RONALD REGAN.

GEORGE HERBERT WALKER BUSH amefariki ikiwa ni miezi saba tu baada ya kifo cha mke wake BARBARA.

Bendera ya Ikulu ya Marekani (White House) zinapepea nusu mlingoti huku mipango ya mazishi ikiendelea.

Rais huyu wa 41 wa Marekani aliongoza muungano wa mataifa mbalimbali kumkabili Saddam Hussein wa Iraq na majeshi yake kutoka Kuwait, lakini akashindwa katika uchaguzi wa awamu ya pili na Rais Bill Clinton mwaka 1992, na kushindwa kumalizia kazi hiyo iliyokuja kumalizwa na mwanaye GEORGE W BUSH aliyeongoza taifa hilo kubwa kwa mihula miwili tangu mwaka 2001 hadi 2009.

Comments

comments