Kukamilika kwa ujenzi wa rada nne za kisasa katika viwanja vinne vya ndege nchini Tanzania kutasaidia kuifanya anga ya Tanzania kuwa salama zaidi na hivyo kuruhusu ndege za mashirika mengi ya nje kutua nchini, hali itakayoongeza mapato ya Serikali.

Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania TCAA inasimamia mradi wa kufunga rada nne za kisasa katika viwanja vya vya ndege vya Julius Nyerere (JNIA), Kilimanjaro (KIA), Mwanza na Songwe, mradi unaogharimu Shs Bilioni 67.3.

Jijini Dar es salaam, timu ya waandishi wa habari iliyokuwa kwenye semina maalumu ya masuala ya usafiri wa
anga,ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya usafiri wa Anga, imetembelea mitambo ya kuongozea ndege na eneo inapojengwa rada mpya ya kisasa.

Awali, Mkuu wa Chuo cha Usafiri wa Anga CATC, Aristid Kanje aliwasilisha mada kwa wanahabari hao kuhusu changamoto za kuwapata wataalamu wa sekta hiyo.

Comments

comments