Kura zimeanza kuhesabiwa baada ya uchaguzi wa rais uliofanyika hapo jana nchini Nigeria, huku watu wengi wakiwa wamechelewa kupiga kura kutokana na matatizo ya uhaba wa wahudumu na hitilafu za teknolojia.

Kura zimeanza kuhesabiwa baada ya uchaguzi wa rais uliofanyika hapo jana nchini Nigeria, huku watu wengi wakiwa wamechelewa kupiga kura kutokana na matatizo ya uhaba wa wahudumu na hitilafu za teknolojia ambapo matokeo rasmi yanatarajiwa kutangazwa mapema wiki ijayo.

Rais ambaye yuko madarakani kwa sasa Mohammadu Buhari alikuwa miongoni mwa watu wa kwanza kupiga kura katika mji wake wa uzawa wa Daura ambapo Mpinzani wake mkubwa Atiku Abubakar alipiga kura katika mji wa Yola, kaskazini mashariki mwa jimbo la Adamawa.

Muda mfupi kabla ya watu kuanza kupiga kura askari mmoja aliuliwa kwenye shambulizi la bomu lililofanywa na magaidi wa Boko Haram katika mji wa Maiduguri kaskazini mashariki mwa Nigeria.

Imeipotiw akwamba pia kulikuwa na mapigano pia katika mikoa ya Yobe na Borno huku kukiwepo na taarifa kwamba watu 16 waliuawa katika vurugu za uchaguzi kwenye majimbo mengine nane nchini umo.

Comments

comments