Mabingwa wa Ligi Kuu Bara, Simba wamefanya mazoezi yao ya kwanza wakiwa nchini Eswatini,Simba wako nchini humo tayari kuwavaa Mbabane Swallows katika mechi ya pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Katika mchezo wa kwanza, Simba walishinda kwa mabao 4-1 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam hivyo wanalazimika kupata ushindi au sare ili kusonga mbele katika mechi itakayochezwa kesho.

Mshambuliaji wao mahiri raia wa Rwanda, Meddie Kagere amesema kuwa wamekwenda Eswatini kutafuta ushindi katika mchezo huo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Mbabane Swallows.

Mchezo huo unatarajiwa kuanza Saa 9:30 kwa saa za huko na saa moja zaidi kwa saa za Afrika Mashariki na utachezeshwa na refa Nelson Emile Fred atakayesaidiwa na washika vibendera Hensley Danny Petrousse na Gerard Pool, wote wa Shelisheli.

Simba itakuwa na kazi nyepesi kesho ikihitaji hata sare kusogea mbele kwenye michuano hiyo baada ya ushindi wa mabao 4-1 kwenye mchezo wa kwanza Jumatano iliyopita Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.

Ushindi huo uliotokana na mabao ya Nahodha John Bocco mawili na wageni, Mnyarwanda Meddie Kagere na Mzambia Clatous Chama unawapa mzigo wa kushinda 3-0 kesho Mbabane ndiyo wasonge mbele.

Jana kikosi cha Simba kilifanya mazoezi mepesi mjini humo baada ya kuwasili ili kuwaondolea uchovu wachezaji wake baada ya safari Tayari kocha Mbelgiji, Patrick. Aussems amesema anatarajiwa mechi ya marudiano itakuwa ngumu Mbabane Swallows wakicheza kwao, lakini wamejipanga vizuri kuhakikisha wanapata matokeo mazuri na kusonga mbele.

Comments

comments