Madiwani wamestushwa na kuhoji ya kiwango cha matumizi ya mafuta katika kipindi cha miezi mitatu wilayani Uvinza

qq

MADIWANI wa Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza, wamestushwa na kuhoji ya kiwango cha matumizi ya mafuta katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita huku wakitaka maelezo ya mchanganuo wa matumizi ya lita elfu 15 za mafuta.

Hayo yameibuka katika kikao cha baraza la madiwani wa halmashauri hiyo mara baada ya madiwani hao kupitia taarifa ya idara ya manunuzi na kubaini matumizi mabaya ya mafuta kwa idara ya afya pekee katika kipindi cha muda wa miezi mitatu yalifikia lita elfu saba,ikilinganishwa na takribani lita elfu tatu zilizotumika katika kipindi kilichopita.

Hatua hiyo imewalazimu afisa wa idara ya manunuzi pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza, kusimama ili kutoa ufafanuzi juu ya suala hilo.

Comments

comments