Majeshi ya Iraq yanaendelea kusonga mbele kuelekea mji wa Hawijah

we

Majeshi ya Iraq jana yaliendelea kusonga mbele kwenye hatua ya pili ya operesheni yake kuukomboa mji wa Hawijah ambao ni ngome ya kundi la IS, na kutwaa vijiji 16 karibu na mji huo.

Jeshi la Iraq, kikosi cha kupambana na ugaidi cha komando na wanamgambo wa Hashd Shaabi walisonga mbele kuelekea kusini mwa mji wa Hawijah, kilometa 230 kutoka mji wa Baghdad na kuvikomboa vijiji hivyo 16.

Waziri mkuu wa Iraq Bw Haider al-Abadi alitangaza kuanza kwa operesheni ya pili ya kuwaondoa wapiganaji wa kundi la IS kutoka kwenye ngome yao mjini Hawijah na maeneo ya karibu ya sehemu ya magharibi ya Kirkuk, kama serikali ilivyoahidi kukomboa ardhi yote ya Iraq kutoka kwa kundi la IS.

CHANZO : CRI KISWAHILI

Comments

comments