Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan amekataza utumiaji wa madalali katika biashara ya mahindi ili kuepuka vitendo vya unyonyoji kwa wakulima vinavyofanywa na madalali hao

Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan amekataza utumiaji wa madalali katika biashara ya mahindi ili kuepuka vitendo vya unyonyoji kwa wakulima vinavyofanywa na madalali hao pamoja na wafanyabiashara wasiowaaminifu.

Mama Samia Suluhu Hassan anaitoa katazo hilo akiwa katika eneo la soko la kimataifa la mazao endagaw wilaya ya Hanang katika muendelezo wa ziara yake ya kikazi mkoani manyara ambapo ameelezwa madalali ndiyo wamekuwa wakitumika katika kuwaunganisha wananchi wakulima na wanunuzi wa zao la mahindi.

Pamoja na kutembelea soko hili makamu wa rais pia ametembelea shule ya wasichana ya Nangwa na kuelezwa na mkuu wa mkoa wa manyara Alexander Mnyeti juu ya uwepo wa ubadhirifu wa milioni mia nane zilizotolewa na serikali kupitia wizara ya elimu kwaajili ya ukarabati wa vyumba kumi vya madarasa hali ambayo imeelezwa kuwa mradi hauendani na gharama halisi hivyo makamu wa rais mama samia suluhu hassan akaeleza kuwa serikali haitatoa fedha nyingine kwaajili ya ujenzi wa bweni jipya shuleni nangwa hadi hapo serikali ijiridhishe na matumizi ya milioni hizo mia nane licha ya kuombwa fedha za ujenzi wa bweni lingine jipya kupitia taarifa iliyosomwa kwake na mkuu wa shule hii.

Pia akiwa eneo la basoutu samia suluhu hassan ameonya wananchi wanaofanya shughuli mbalimbali ikiwemo za kilimo pembezoni mwa vyanzo vya maji ikiwemo ziwa basoutu huku pia akizindua mradi wa maji wenye dhamani ya zaidi ya bilioni mbili kwa manufaa ya wananchi wa vijiji nane eneo la basoutu wilaya ya Hanang.

Comments

comments