Makamu wa Rais mama Samia Suluhu Hassan amewasili jijini Kampala, Uganda kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa mwaka 2019 wa ‘Africa Now Summit’ unaotarajiwa kufanyika kesho na kesho kutwa.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewasili jijini Kampala, Uganda kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa mwaka 2019 wa ‘Africa Now Summit’unaotarajiwa kufanyika kesho na keshokutwa. Makamu wa Rais atamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwenye mkutano huo.

Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Ndege wa Entebbe, Makamu wa Rais amelakiwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Philemon Mateke pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Uganda Dkt. Aziz Mlima.

Makamu wa Rais amefuatana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Damas Ndumbaro.

Mkutano wa mwaka 2019 wa “Africa Now Summit 2019” utafunguliwa kesho na Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni ambapo viongozi mbalimbali wa Afrika wanakutana ili kupata majibu ya changamoto za Afrika katika masuala ya kiuchumi.

Viongozi wengine watakaotoa mada kwenye mkutano huo ni Rais wa Misri ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (UA) Abdel Fattah el Sisi; Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa; Makamu wa Rais wa Kenya William Ruto; na Waziri Mkuu wa Ethiopia Ahmed Abiy pamoja na Rais Paul Kagame wa Rwanda.

Comments

comments