Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema ili kuibadili Afrika Viongozi wake lazima wawekeze kwa Vijana na Watoto.

Makamu wa Rais ameyasema hayo wakati akihutubia kwenye mkutano wa Africa Now Summit 2019 jijini Kampala nchini Uganda.

Amesisitiza kwamba viongozi lazima wawekeze kwenye Lishe bora ya watoto wanaozaliwa na kuhakikisha mifumo ya elimu inalenga kutoa elimu bora na zenye kukuza vipaji ili kwenda sambamba na ulimwengu wa teknolojia.

Aidha Makamu wa Rais amesisitiza Afrika lazima iwekeze kwenye mipango itakayoleta maendeleo endelevu kwa vizazi vijavyo na si mipango kwa ajili ya chaguzi zijazo.

Mkutano huo uliofunguliwa na Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni una lengo la kuwakutanisha Viongozi wa Afrika kujadili masuala mbalimbali ya utengamano katika kuleta maendeleo endelevu barani Afrika.


Comments

comments