Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa wakulima wa alizeti mkoani Singida kutumia mkopo walioupata kutoka Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB).

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa wakulima wa alizeti mkoani Singida kutumia mkopo walioupata kutoka Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) ili kuendeleza uzalishaji wa mazao ya kimkakati mkoani humo.

Makamu wa Rais ametoa wito huo wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara wa kukabidhi hundi ya mfano yenye thamani ya Shilingi 1.285 Billioni zilizotolewa na TADB kwa ajili ya miradi ya kilimo cha Alizeti kwa wakulima 458 waliochini ya vyama vya ushirika (AMCOS) mkoani Singida.

Awali akimkaribisha Makamu wa Rais mjini Manyoni, Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Rehema Nchimbi ameshukuru TADB kwa kutoa mkopo kwa AMCOS hizi saba mkopo ambao umelenga kuongeza tija ya uzalishaji wa alizeti mkoani humo.

Akizungumza kwa niaba ya wakulima wa Alizeti walionufaika na mkopo huo, Makamu Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika Singida, Yahya Ramadhan amesema ujio wa Benki ya Kilimo umerudisha ari ya wakulima wa zao la alizeti mkoani Singida.

Comments

comments