Shambulio la mtandao, Mamlaka nchini Marekani kufanya uchunguzi

hacker-attack

Mamlaka nchini Marekani imesema inachunguza shambulio kubwa la kimtandao ambalo limekumba mifumo ya kompyuta duniani kote.

Baraza la Taifa la Usalama jijini Washington limesema Marekani imedhamiria kuwachukulia hatua wahusika wa uhalifu huo wa mtandaoni.

Mashirika mbalimbali ikiwemo taasisi za kifedha, idara za serikali, makampuni makubwa, na kampuni za usafirishaji ni miongoni mwa yaliyoathirika na shambulizi la mtandao.

Watumiaji wameambiwa komputa zao zimenasa mpaka walipe kiasi cha dola mia tatu katika akaunti isiyofahamika ambapo hata hivyo wizara ya mambo ya ndani ya Marekani imewashauri watu wasilipe fedha hizo.

Shambulio hilo la kimtandao lilianza nchini Ukraine na linaendelea sehemu nyengine duniani kote ambapo linatarajiwa kuathiri mataifa mengi.

Comments

comments