Umoja wa Mataifa umesema walinda amani wake wapatao 7 wameuawa katika mapigano yaliyozuka karibu na mji wa Beni kaskazini mwa Kivu, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya tukio hilo, msemaji wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric amesema wanajeshi hao waliokufa, 6 ni kutoka Malawi na 1 Tanzania. Bado haijajulikana ni kundi gani la waasi limehusika na mashambulizi hayo

Stephane Dujarric amesema Walinda amani hao wameuawa wakati wa operesheni ya pamoja iliyokuwa ikifanywa na Kikosi cha Kulinda amani cha Umoja wa Mataifa na Jeshi la Congo dhidi ya kundi LA Allied Democratic Foirces linalojulikana kama ADF.

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa Taarifa za awali zinaonesha kuwa walinda amani wengine 10 wamejeruhiwa na mmoja hajulikani alipo.

Comments

comments