Maseneta nchini Marekani, baada ya kupewa taarifa ya kina na Mkurugenzi wa taasisi ya Ujasusi CIA, wanasema sasa wanaamini kuwa Mwanamlfalme wa Saudi Arabia, Mohammed Bin Salman, aliagiza kuuawa kwa Mwanahabari Jamal Khashoogi.

Aidha, wamesema wameshangazwa namna serikali ya Marekani ilivyoshughulikia mauaji ya Khashoogi, baada ya Rais Donald Trump kuonekana kuutetea uongozi wa Saudi Arabia.

Seneta mwenye ushawishi mkubwa kutoka chama cha Republican Lindsey Graham amesema ana “imani ya hali ya juu” kuwa Mohammed bin Salman (MBS) alipanga njama ya kumuua Khashoggi.

Khashoggi ambaye alikuwa ni mkosoaji mkubwa wa sera za Saudia hususani mwanamfalme bin Salman, aliuawa ndani ya ofisi za ubalozi mdogo wa Saudi Arabia jijini Istanbul, Uturuki Oktoba 2.

Mwanahabari huyo alikuwa ni mkosoaji mkubwa wa sera za Saudia hususani mwanamfalme bin Salman.

Wakati hayo yakijiri mwendesha mashtaka mku nchini Uturuki ametoa hati yakukamatwa kwa wasaidizi wawili wa Mwana wa mfalme wa Saudi Arabia ambapo hati hiyo pia inahusisha mkuu wa upelelezi wa nje wa nchi hiyo kwa kupanga na kutekeleza mauaji ya mwandishi wa habari Jamal Khashoggi.

Comments

comments