Mashirika ya haki za binadamu nchini Nigeria yameripoti kuwa zaidi ya watu 40 wameuawa katika vurugu zilizoikumba Nigeria hapo jana wakati wa shughuli ya kuhesabu kura ikiendelea kufuatia uchaguzi uliofanyika siku ya Jumamosi nchini humo.

Ingawa Taarifa hiyo iliyotolewa na Mashirika hayo ya haki za binadamu haijathibitishwa na vyombo vya Dola vya Nigeria lakini Polisi nchini humo imethibitisha kuwakamata watu zaidi ya 28 kutokana na kuhusika katika matukio ya vurugu yanayohusishwa na uchaguzi ambayo yamesababisha watu kadhaa kujeruhiwa huku wengine wakipoteza maisha.

Rais wa sasa Muhammadu Buhari mwenye umri wa miaka 76 anatafuta muhula wa pili wa uongozi ambapo anapambana na Atiku Abubakar mwenye umri wa miaka 72, mfanyabiashara na makamu wa rais wa zamani.

Matokeo rasmi ya uchaguzi huo yanatarajiwa kuanza kutangazwa leo licha ya maeneo mengine yalipiga kura hadi siku ya jana huku wagombea Buhari na Abubakar wakidai kushinda uchaguzi huo

Zaidi ya watu milioni 72 walisajiliwa kupiga kura katika taifa hilo lenye idadi kubwa kabisa ya watu barani Afrika na ambalo lina uchumi mkubwa.

Comments

comments