Mchumi na mhadhiri kutoka Chuo Kikuu Mzumbe Profesa Honest Prosper Ngowi amepongeza makadirio ya Bajeti kwa mwaka 2019/20 pamoja na vipaumbele vyake pamoja na kusisitiza umuhimu wa kuendelea kukuza mapato ya ndani.

Mchumi na mhadhiri kutoka Chuo Kikuu Mzumbe Profesa Honest Prosper Ngowi amepongeza makadirio ya Bajeti kwa mwaka 2019/20 pamoja na vipaumbele vyake pamoja na kusisitiza umuhimu wa kuendelea kukuza mapato ya ndani ili nchi iweze kujitegemea na kupunguza au kuachana kabisa na fedha za wahisani.

Akitoa uchambuzi wa makadirio ya bajeti hiyo Profesa Honest Prosper Ngowi amesema vipaumbele vilivyowekwa na mwelekeo mzima wa bajeti hiyo ni mzuri ambapo amesisitiza kikubwa ni kusimamia upatikanaji wa fedha hizo na kuhakikisha miradi iliyopangwa inatekelezwa.

Akizungumza kuhusu utekelezwaji wa ahadi za wahisani kwa kiwango cha asilimia 69 kwa kipindi cha nusu mwaka wa fedha 2018/19 amesema ni hatua nzuri inayoashiria kuridhishwa kwao na utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa nchini na serikali ya awamu ya tano.

Wiki hii waziri wa fedha na mipango Dkt. Philip Mpango aliwasilisha taarifa mjini Dodoma kuhusiana na mwelekeo wa bajeti, ambapo alisema makadirio ya mapato na matumizi katika mwaka ujao wa fedha wa 2019/20 yanatarajiwa kuwa shilingi trilioni 33.1 huku mapato ya ndani yakiwa shilingi trilioni 23.

Comments

comments