Mfululizo wa video zinazotengenezwa kwa kufuata nukuu anazopenda rais wa China watangazwa duniani

Kabla ya Rais Xi Jinping wa China kuhudhuria Mkutano wa kilele wa G20 na kufanya ziara nchini Argentina, mfululizo wa video za lugha ya Kihispania zilizotengenezwa kwa kufuata nukuu anazopenda rais Xi, zimetangazwa katika nchi zinazozungumza lugha ya kihispania kote duniani kuanzia tarehe 29. Sherehe ya uzinduzi pia ilifanyika siku hiyo mjini Buenos Aires, Argentina.

Tarehe 28 Kituo Kikuu cha Radio na Televisheni cha Taifa cha China kikishirikiana na Kituo cha Radio na Televisheni cha Argentina pia zimefanya shughuli za kuzitangaza.

Video hizo mfululizo zitaoneshwa kupitia vyombo vikubwa vya habari katika nchi nyingi zinazozungumza lugha ya kihispania zikiwemo Argentina na Hispania, tovuti za jumuiya za washauri bingwa kama Kituo cha utafiti wa masuala ya siasa na uchumi nchini Argentina, pamoja na vituo vya televisheni na radio, APP na mtandao wa kijamii inayotumia lugha ya kihispania zinazomilikiwa na Kituo Kikuu cha Radio na Televisheni cha Taifa cha China.

Video hizo zilizotafsiriwa na Kituo Kikuu cha Radio na Televisheni cha Taifa la China kwa lugha za kiingereza, kijapani, na Kikorea, zimefuatiliwa na kupongezwa na watazamaji.

 

Katika Sherehe ya uzinduzi ya video hizo iliyofanyika siku hiyo, mkuu wa Kituo Kikuu cha Radio na Televisheni cha Taifa la China Bw. Shen Haixiong ameeleza kuwa, video hizo zimefungua dirisha kwa watazamaji wanaozungumza lugha ya kihispania kumfahamu rais Xi Jinping, na jinsi alivyofanikiwa kuiongoza China ikiwa nchi kubwa zaidi inayoendelea duniani kwenye zama mpya, na kupiga hatua katika kutimiza ustawi wa taifa la China.

Mwanzilishi wa kundi la vyombo vya habari vya la Amerika Bw. Jose Luis Manzano amesema, mfululizo huo wa video umetoa fursa nzuri kwa kufahamu utamaduni wa China. Rais Xi aliyetoa sauti yake yenyewe kupitia video hizo, amefahamisha ushawishi wa nadharia za jadi za China kwa jamii ya binadamu na nchini China. Fikra na utamaduni wa China wenye historia ndefu bado vina umuhimu mkubwa katika kuielekeza dunia ya sasa.

Comments

comments