Mgombea urais wa chama tawala nchini Nigeria aliyekuwa akitetea kiti hicho Rais Muhammadu Buhari ameibuka mshindi wa uchaguzi uliofanyika Jumamosi Februari 23.

Kulingana na matokeo ya awali yaliyotangazwa na Tume ya Uchaguzi (INEC), Buhari amepata asilimia 56 ya kura zote zilizopigwa hivyo kumpa uhalali wa kuiongoza nchi hiyo ya Afrika magharibi kwa miaka mingine minne.

Hata hivyo awali upinzani ulilalamikia kuwepo kwa njama za kuiba kura na kudai kwamba hautokubali matokeo hayo

Habari zinasema Buhari ameshinda kwa kishindo katika majimbo ya Kaskazini, na pia kupata ushindi mkubwa katika Majimbo ya Bauchi, Borno, Yobe, Zamfara na Kaduna. Buhari mwenye umri wa miaka 76 amemshida mpinzani wake mkuu na aliyewahi kuwa makamu wa rais Atiku Aboubakar. Chama cha Buhari kimeshinda katika majimbo 19 kati ya 36 , wakati chama cha upinzani cha PDP wakishinda majimbo 17.

Hata hivyo ni asilimia 35 tu ya wapiga kura walijitokeza kushiriki uchaguzi huo, na tayari baadhi wafuasi wa Buhari i wameingia mtaani kushangilia ushindi huo. Buhari alichaguliwa kwa mara ya kwanza mwaka 2015 akiwa kiongozi wa kwanza wa upinzani kuwa rais.

Comments

comments