Mgombea wa upinzani katika uchaguzi muhimu wa rais unaopangwa kufanyika Disemba 23 DRC, Felix Tchisekedi anaingia katika kinyanganyiro hicho akiwa na ushawishi wa kisiasa kama mwana wa Marehemu Etienne Tshisekedi, mwanzilishi wa chama cha UDPS

Mgombea wa upinzani katika uchaguzi muhimu wa rais unaopangwa kufanyika Disemba 23 nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo Felix Tchisekedi, anaingia katika kinyanganyiro hicho akiwa na ushawishi wa kisiasa kama mwana wa Marehemu Etienne Tshisekedi, mwanzilishi wa chama cha UDPS.

Felix Tshisekedi na Vital Kamerhe ambao walijiondoa katika makubaliano ya Geneva Uswis kuhusu upinzani kuwa na mgombea mmoja ambaye ni Martin Fayulu jana wamekubaliana kuwa Felix ndiye atakayepeperusha bendera ya upinzani.

Hii ina maana kwamba upinzani utakuwa na wagombea wawili ambao ni Martin Fayulu na Felix Tshisekedi ambao watapambana na mgombea wa muungano wa vyama vinavyomuunga mkono rais Kabila FCC katika Uchaguzi Mkuu wa tarehe 23 Desemba, Mwaka huu.

Katika hatua nyingine baraza la maaskofu wa kanisa katoliki wameendelea kuonesha wasiwasi wao kuhusu suala la matumizi ya mashine za kupigia kura huku upande wa chama tawala ukisisitiza kuwa uchaguzi utakaofanyika utakuwa huru na haki.

Comments

comments