Miezi mitatu ijayo ni muhimu kwa China na Marekani, Marais wa China na Marekani walikutana Desemba mosi kando ya mkutano wa kilele wa G20 uliofanyika nchini Argentina, na kufikia makubaliano ya kusitisha hatua za kuongezeana ushuru, na kuamua kuweka muda wa siku tisini ili kutoa nafasi kwa ajili ya majadiliano kati ya pande hizo mbili.

 
Marais wa China na Marekani walikutana Desemba mosi kando ya mkutano wa kilele wa G20 uliofanyika nchini Argentina, na kufikia makubaliano ya kusitisha hatua za kuongezeana ushuru, na kuamua kuweka muda wa siku tisini ili kutoa nafasi kwa ajili ya majadiliano kati ya pande hizo mbili.
 
Hatua hiyo imefikiwa miezi nane baada ya kuanza kwa mgogoro wa kibiashara kati ya China na Marekani, ambao umezisababishia hasara za kiuchumi pande zote mbili.
 
Oktoba 14 rais Donald Trump alipohojiwa na televisheni ya CBS alisema yaliyotokea kati ya China na Marekani sio vita ya kibiashara, na bali ni “mgogoro mdogo”, na alikuwa anafikiria kutuliza mgogoro huo.
 
Hivi sasa wakuu wa China na Marekani wamepiga breki kwenye mkwaruzano kati ya nchi mbili, hatua ambayo ni ya busara na yenye faida kwa pande zote mbili.
 
Katika miezi mitatu ijayo, China itajitahidi kufanya mawasiliano na Marekani kuelekea lengo la kukomesha ushuru, kwenye msingi wa kulinda maslahi ya pamoja na utaratibu wa jumla wa biashara duniani.

Comments

comments