Naibu waziri wa fedha na mipango Dk. Ashatu Kijaji atoa agizo kwa bodi ya wataalam wa manunuzi ya umma (PSPTB) kutatua kasoro ikiwemo rushwa na udanganyifu ili kuepusha hasara kwa taifa.

Naibu waziri wa fedha na mipango Dk. Ashatu Kijaji ameiagiza bodi ya wataalam wa manunuzi ya umma (PSPTB) kutatua kasoro mbalimbali ikiwemo rushwa na udanganyifu ili kuepusha hasara kwa taifa.

Dk. Kijaji ametoa agizo hilo Jijini Dodoma kwenye ufunguzi wa kongamano la tisa la bodi hiyo ambapo amewataka wataalamu hao kujitathimini kutokana na kukithiri kwa vitendo vya rushwa.

Ni kongamano la tisa la bodi ya wataalam wa manunuzi ya umma na ugavi ambalo linafanyika jijini hapa kwa siku mbili na mada kuu inayojadiliwa ni ìUnunuzi Na Ugavi Katika Kuchangia Ujenzi Wa Miundombinu Nchiniî.

Dk. Kijaji anasema ripoti mbalimbali za uchunguzi zikiwemo za PPRA na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali (CAG) zimebaini mapungufu makubwa ya ununuzi usiozingatia sheria na kanuni hali inayolisababishia taifa hasara.

Aidha Dk. Kijaji akazungumzia namna udanganyifu wa thamani ya miradi unavyoathiri mahusiano baina ya serikali na wananchi.

Mwenyekiti wa Bodi ya PSPTB anaipongeza serikali kutokana na waraka uliotolewa na wizara ya fedha na mipango wa kuzitaka taasisi zote za serikali kuajiri wataalam wa ununuzi na ugavi wenye sifa zilizothibitishwa na bodi.

Comments

comments