Migogoro ya ardhi Morogoro, Waandishi wa habari washirikishwa kwenye usuluhishi

rrr

Chama cha waandishi wa habari mkoa wa Morogoro kimeendelea kutoa elimu ya uelishamishaji wa suala la utatuzi wa migogoro ya ardhi, matumizi bora ya ardhi na utambuzi wa sheria za ardhi ili kuhamasisha amani licha ya kazi ya kuandika habari za Migogoro hiyo kwa muda mrefu.

Mratibu wa mafunzo ya uhamasishaji swala la utatuzi wa migogoro ya ardhi kutoka chama cha waandishi wa habari mkoa wa Morogoro Merina Robart amesema kuwa nia ya waandishi wa habari kuendesha zoezi hilo ni katika kuungana na serikali ili kuhamasisha amani na utulivu katika jamii ya wakulima na wafugaji juu ya migogoro ya ardhi licha ya kuwa wameripoti habari hizo kwa kipindi kirefu na kuamua kuja na majibu ya tatizo hilo.

Washiriki wa mafunzo hayo wamesema kuwa elimu hiyo iendelee kutolewa kwani wameufaika nayo na kutambua mambo mengi ambayo yanatakiwa yafatwe katika mpango bora wa matumizi ya ardhi na kujua sheria itakayo wasaidia kupata haki zao.

Comments

comments